KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, July 27, 2012

KABURU:TIMU YA SIMBA NI NZURI MAZOEZI KUANZA JUMATATU.


Baada ya kuondolewa kwenye hatua ya Robo fainali ya michuano ya kombe la Kagame , wabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wanatarajia kurejea mazoezini jumatatu kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya bara .
Akizungumza na Rockersports Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Geofrey Nyange Kaburu amesema kocha mkuu wa timu hiyo Milovan Circovic aliwapa mapumziko ya siku nne wachezaji wote walioshiriki michuano ya kombe la kagame isipokuwa wale tu ambao hawakuwemo kwenye kikosi cha kagame ambao wenyewe wanaendelea na mazoezi ya Gym.
Mbali ya wachezaji hao kocha Milovan amechukua mapumziko ya siku tano kurejea kwao lakini kikosi chote cha simba kikitakiwa kurejea mazoezini jumatatu.
Kaburu amesema baada ya kushindwa kusonga mbele kwenye michuano ya kagame inayomalizika hapo kesho tayari kocha wao ameshawakabidhi ripoti yake na wao kama viongozi wanaifanyia kazi.

Ameongeza kuwa kama uongozi wamesikitishwa kwa timu yao kutofanya vizuri kwenye michuano ya kagame lakini ifahamike kuwa simba inawachezaji wapya ambao wanajaribiwa kwa ajili ya usajili kamili.
Mbali ya hivyo kaburu pia amesema tangu mapema kocha wao alishauambia uongozi kuwa licha ya kushiriki michuano ya kombe la kagame lakini alikuwa bado hakifahamu kikosi hicho kutokana na ukweli kuwa hakuwa pamoja nacho kwa muda mrefu.
Kaburu amesema anaamini simba bado inakikosi kizuri tatizo ni kuwa wachezaji bado hawajachanganya , amewatoa hofu mashabiki wa simba kwa kusema simba itatisha kwani hata wakati wa ligi kuu wakiwa na wachezaji nyota kama vile Emmanuel Okwi pamoja na Marehemu Patrick Mafisango Simba ilifungwa bao moja kwa bila na timu iliyokuwa ikiburuza mkia katika ligi kuu Villa squad lakini hatimaye simba ikatwaa ubingwa.
Ameongeza kuwa  ripoti ya kocha wao imeelezea mambo mbalimbali yanayotakiwa kufanyiwa kazi  na wao viongozi wameikabidhi kwa kamati ya ufundi waifanyie kazi.
Amesema kuwa kwa sasa hawawezi kuzungumzia suala zima la usajili kama watakifanyia marekebisho kikosi chao kutokana na kuboronga kwenye michuano ya kombe la kagame kama wadau wa timu hiyo wanavyotaka.
Akizungumzia  kama kuna wachezaji wamewaona na wanafaa kusajiliwa na simba ndani ya Michuano ya kombe la Kagame Kaburu amesema,
 Kimsingi michuano ya Kagame ilikuwa na wachezaji wazuri lakini simba pia ina wachezaji wazuri isipokuwa bado hawajachanganya vizuri lakini kama kutakuwa na mapendekezo yoyote ya kufumua kikosi, basi watafanya hivyo kwani usajili bado unaendelea.
Aidha kaburu ametumia nafasi ya kuzungumza na Rockersport kuzipongeza timu zote zilizotinga hatua ya ya fainali kwa kusema kuwa zimepigana kiume kufikia hatua hiyo.

2 comments:

  1. Tunataka timu iingie kambini mapema ili mapungufu makubwa tuliyoyaona yafanyiwe tarehe 25 sio mbali tunakutana na azam fc tena, pia mawazo yangu bado naona Machaku anatufaa sana.

    by mshabiki mkubwa wa MNYAMA(Andy)

    ReplyDelete
  2. Tunataka timu iingie kambini mapema ili mapungufu makubwa tuliyoyaona yafanyiwe kazi haraka tarehe 25/08 sio mbali tunakutana na azam fc tena, pia mawazo yangu bado naona Machaku anatufaa sana.

    by: mshabiki mkubwa wa MNYAMA(Andy)

    ReplyDelete