Baada ya
kuondolewa kwenye hatua ya Robo fainali ya michuano ya kombe la Kagame , wabingwa
wa soka Tanzania Bara Simba wanatarajia kurejea mazoezini jumatatu kwa ajili ya
kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya bara .
Akizungumza
na Rockersports Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Geofrey Nyange Kaburu amesema kocha mkuu wa timu hiyo Milovan Circovic aliwapa mapumziko ya siku nne
wachezaji wote walioshiriki michuano ya kombe la kagame isipokuwa wale tu ambao
hawakuwemo kwenye kikosi cha kagame ambao wenyewe wanaendelea na mazoezi ya
Gym.
Mbali ya
wachezaji hao kocha Milovan amechukua mapumziko ya siku tano kurejea kwao
lakini kikosi chote cha simba kikitakiwa kurejea mazoezini jumatatu.
Kaburu
amesema baada ya kushindwa kusonga mbele kwenye michuano ya kagame
inayomalizika hapo kesho tayari kocha wao ameshawakabidhi ripoti yake na wao
kama viongozi wanaifanyia kazi.
Ameongeza kuwa
kama uongozi wamesikitishwa kwa timu yao kutofanya vizuri kwenye michuano ya
kagame lakini ifahamike kuwa simba inawachezaji wapya ambao wanajaribiwa kwa
ajili ya usajili kamili.
Mbali ya
hivyo kaburu pia amesema tangu mapema kocha wao alishauambia uongozi kuwa licha
ya kushiriki michuano ya kombe la kagame lakini alikuwa bado hakifahamu kikosi
hicho kutokana na ukweli kuwa hakuwa pamoja nacho kwa muda mrefu.
Kaburu
amesema anaamini simba bado inakikosi kizuri tatizo ni kuwa wachezaji bado
hawajachanganya , amewatoa hofu mashabiki wa simba kwa kusema simba itatisha
kwani hata wakati wa ligi kuu wakiwa na wachezaji nyota kama vile Emmanuel Okwi
pamoja na Marehemu Patrick Mafisango Simba ilifungwa bao moja kwa bila na timu
iliyokuwa ikiburuza mkia katika ligi kuu Villa squad lakini hatimaye simba
ikatwaa ubingwa.
Ameongeza kuwa
ripoti ya kocha wao imeelezea mambo
mbalimbali yanayotakiwa kufanyiwa kazi
na wao viongozi wameikabidhi kwa kamati ya ufundi waifanyie kazi.
Amesema kuwa
kwa sasa hawawezi kuzungumzia suala zima la usajili kama watakifanyia
marekebisho kikosi chao kutokana na kuboronga kwenye michuano ya kombe la
kagame kama wadau wa timu hiyo wanavyotaka.
Akizungumzia kama kuna wachezaji wamewaona na wanafaa
kusajiliwa na simba ndani ya Michuano ya kombe la Kagame Kaburu amesema,
Kimsingi michuano ya Kagame ilikuwa na wachezaji
wazuri lakini simba pia ina wachezaji wazuri isipokuwa bado hawajachanganya vizuri
lakini kama kutakuwa na mapendekezo yoyote ya kufumua kikosi, basi watafanya
hivyo kwani usajili bado unaendelea.
Aidha kaburu
ametumia nafasi ya kuzungumza na Rockersport kuzipongeza timu zote zilizotinga
hatua ya ya fainali kwa kusema kuwa zimepigana kiume kufikia hatua hiyo.
Tunataka timu iingie kambini mapema ili mapungufu makubwa tuliyoyaona yafanyiwe tarehe 25 sio mbali tunakutana na azam fc tena, pia mawazo yangu bado naona Machaku anatufaa sana.
ReplyDeleteby mshabiki mkubwa wa MNYAMA(Andy)
Tunataka timu iingie kambini mapema ili mapungufu makubwa tuliyoyaona yafanyiwe kazi haraka tarehe 25/08 sio mbali tunakutana na azam fc tena, pia mawazo yangu bado naona Machaku anatufaa sana.
ReplyDeleteby: mshabiki mkubwa wa MNYAMA(Andy)