KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, July 20, 2012

Mgongolwa: Kelvin Yondani ruksa Yanga



Kamati ya sheria, hadhi na wachezaji ya shirikisho la soka nchini TFFimemruhusu mlinzi wa zamani wa mabingwa wa soka Tanzania bara Simba Kelvin yondani kuendelea kuichezea timu ya Yanga katika michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea hivi sasa jijini Dar es Salaam
Akizungumza hii leo na waandishi wa habari mwenyekiti wa kamati hiyo Alex Mgongolwa amesema maamuzi ya sekretarieti ya TFF  kumruhusu yondani kuichezea Yanga yliyofanywa na katibu wa TFF Angetile Oseah ni maamuzi sahihi kwa kuwa mkataba wa Simba na Yondani umemalizika May 31 mwaka huu.
Mgongolwa amesema Yondani tangu tarehe hiyo alikuwa huru na kwamba Simba waliwasilisha TFF ombi la kumuongezea mkataba Yondani June 7 ambapo ni kinyume na taratibu za kuongezea mkataba kwa mchezaji hivyo Yondani ruksa kuichezea Yanga.
Aidha katika kuonyesha wapi mkanganyiko wa mkataba wa Yondani ulipoanzia Mgongolwa amesema mkataba wapili wa Simba unaonyesha umesainiwa desemba 23 mwaka huu muda ambao haujafika hivyo hauna athari kwa Yondani kutokuichezea Yanga kwenye michuano ya Kagame.

Hata hivyo kamati hiyo imetoa rai kwa Simba na Yondani kukaa chini na wakubaliane kuhusu mkataba huo wenye makosa.
Yondani


1 comment:

  1. haki imetendeka wazee wa kufoji mikataba poleni.waandaeni yoso wenu wazibe pengo badala ya kumng'ang'ania yondani

    ReplyDelete