Makamu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga mwenye koti |
Viongozi wa
matawi wa klabu ya Yanga wamekutana hii
leo katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko matika makutano ya mitaa Twiga na
Jangwani Kariakoo jijini Dar es salaam kwa lengo la kujadili juu ya mipango ya
kuimaliza APR ya Rwanda mchezo wa nusu fainali wa michuano ya kombe la Kagame
kesho katika uwanja wa taifa.
Mkutano huo
ulioitishwa na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga ulikuwa na ajenda
kuu moja nayo ni kuhusu namna ya kumalizia michezo miwili ya kombe la Kagame na
hatimaye klabu hiyo kufanikisha azma ya kutetea taji hilo.
Yanga
imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya juzi kuitoa
kwa penati timu ngumu ya Mafunzo katika mchezo wa robo na sasa ikisubiri
kukabiliana na mabingwa wa soka wa Rwanda APR mchezo ambao utatanguliwa na
mchezo mwingine wa hatua hiyo ambao Azam fc itakuwa ikicheza dhidi ya timu
alikwa ya Vita Club ya DRC.
Katika
mkutano wa leo viongozi hao wa matawi wamekubaliana kimsingi kuunganisha nguvu
zao katika kila hali ili kufanikisha lengo hilo.
Sanga
amesema wao kama viongozi wapya wa Yanga bado hawajakaa kama kamati ya utendaji
mbali na ukweli kuwa ni wageni katika kuingoza klabu hiyo kongwe hapa nchini,
hivyo aliona ni vema kuwaita viongozi hao kujadiliana kwa pamoja namna ya
kulinda taji hilo pale Jangwani.
Amewataka
wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kuiombea timu yao lakini pia wajitokeze kwa
wingi kuishangilia na kuipa nguvu timu hiyo katika mchezo wa kesho ili waweze
kuingia fainali na hatimaye kutwaa taji hilo.
No comments:
Post a Comment