KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, July 12, 2012

KAGAME CUP :NSAJIGWA NJE, MSUVA,DUMAYO OMEGA KUKOSA MCHEZO WA KWANZA WA YANGA


Thom Saintfiet
KOCHA wa klabu ya Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet amemtema nahodha wa timu hiyo Shadrack Nsajigwa katika kikosi chake cha wachezaji 20 ambacho kitakuwa kikitetea ubingwa wa michuano ya Kombe la Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, kocha huyo amesema kuwa mbali ya Nsajigwa pia amewaacha wachezaji watatu ambao wamo katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 ya Tanzania-Ngorongoro Heroes katika michezo ya hivi karibuni inayowakabili.
Wachezaji hao chipukizi ni Omega Seme, Simon Msuva na Frank Damayo ambao watakuwemo katika kikosi cha Ngorongoro ambacho Jumamosi kitakuwa na mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Rwanda na kurudiana nao tena Jumatatu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Nigeria unaotarajiwa kuchezwa Julai 29 mwaka huu.
Kocha huyo amesema kuwa pamoja na kumtema Nsajigwa katika kikosi hicho lakini mchezaji huyo bado ni muhimu katika timu hiyo na ameamua kumpa nafasi ya kujiweka fiti kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambako atamtumia.
Kikosi kamili cha Yanga ambacho kitashiriki Kagame kitakuwa na makipa Yaw Berko na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki watakuwa Juma Abdul, David Luhende, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Godfrey Taita, Ladislaus Mbogo, Oscar Joshua na Stefano Mwasika.
Wengine ni viungo Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo, Juma Seif ‘Kijiko’, Haruna Niyonzima, Shamte Ally, Nizar Khalfan na Idrisa Assenga wakati washambuliaji watakuwa ni Said Bahamuzi, Hamis Kiiza na Jerry Tegete.
Saintfiet amesema kuwa kiungo Nurdin Bakari naye ametemwa katika kikosi hicho kutokana majeraha yanayomsumbua ambapo daktari wa timu amesema ataweza kuwa fiti baada ya wiki mbili wakati ambao michuano ya Kagame itakuwa tayari imeshaanza ndiyo sababu kubwa ya kuachwa.

No comments:

Post a Comment