Federico Macheda |
Federico
Macheda alifunga bao pekee la Manchester United dhidi ya AmaZulu wakati timu
hiyo ikianza ziara ya matayarisho ya msimu mpya wa ligi 2012/2013 nchini Afrika
Kusini.
mshambuliaji
huyo Mtaliano alifunga goli hilo akiwa pembeni mwa uwanja kunako dakika ya 19.
lakini
katika mchezo huo United ilikuwa ikishambiliwa sana kiasi mlinda mlango Anders
Lindegaard akilazimika kuokoa michomo kadhaa ikiwemo mpira wa kichwa wa Josef
Letka.
Shinji
Kagawa kiungo mpya wa timu hiyo aliingizwa zikiwa zimebakia dakika mbili mpira
kwisha.
Bosi wa United
Sir Alex aliwatumia wazoefu katika timu yake kama vile Rio Ferdinand, Paul
Scholes, Michael Carrick, Javier Hernandez na Dimitar Berbatov anajaribu
kutafuta kiwa cha kiushindani zadi katika kipindi hiki cha maandalizi ya kuanza
ligi ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment