KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, July 26, 2012

TFF NA MASHINDANO MAPYA.

Shirikisho la soka nchini Tff limeingia mkataba wa miaka mitatu na BancABC kwa ajili ya kuandaa mashindano yenye lengo la kuziandaa timu mbalimbali kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu za Tanzania Bara na Zanzibar (yaani pre season) ambayo yatakuwa yakiitwa BancABC sup8r Soccer tournament 2012.
Wakiongea hii leo mbele ya waandishi wa habari katibu wa TFF Angetile Oseah na mkuu wa kitengo cha fedha wa banki ya ABC Mwalimu Zuberi aliyeambatana na mkurugenzi wa benki hiyo Bornface Nyoni wamesema lengo kuu la mashindano hayo ni kutoa zawadi kwa wateja wa benki yao mbali ya kutoa burudani lakini pia ni kutimiza tamko la serikali kwa wawekezaji makampuni na taasisi binasfi kujihusisha na michezo.
Mashindano hayo ambayo kwa mwaka huu yamepangwa kufanyika kuanzia August 4 mpaka 18 yatakuwa yakifanyika katika vituo vinne vya Dar es Salaam , Arusha ,Mwanza na Zanzibar na yatakuwa yakishirikisha jumla ya timu nane ambazo ni zile zilizo shika nafasi tatu za juu katika ligi kuu ya Vodacom(Tanzania Bara) na nyingine tatu za juu katika ligi ya Zanzibar.
Timu nyingine ni mbili ni zile zilizo panda daraja toka kila upande moja kutoa Tanzania Bara na nyingine kutoka Zanzibar.
Mkataba wa TFF na Benki hiyo ni wa miaka 3 lakini hata hivyo haijawekwa wazi unathamani ya kiasi gani kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kutakuwa na mabadiliko kila mwaka.
Katibu wa TFF Angetile Oseah amesema tayari amesha viandikia barua vilabu vyote kuwajulisha juu ya hilo licha ya kushindwa kuthibitisha juu ya kama wamekubalia ama la.

No comments:

Post a Comment