VS
Wagombea wa uongozi katika klabu ya Yanga hii leo wameshindwa kuanza kampeni kutokana na kamati ya uchaguzi ya shirikisho la kandanda nchini Tanzania TFF kushindwa kukamilisha kazi ya kuhakiki vyeti halisi vya baadhi ya wagombea waliotakiwa kufanya hivyo ili kuthibtisha uhalali wa vivuli vya vyeti vyao.
Yanga ilipanga kuzindua kampeni kwa wanachama wake wanaotaka kujaza nafasi za uongozi zilizo achwa wazi na wajumbe wa wakati ya utendaji waliojiuzulu chini ya aliyekuwa mwenyekiti wakati huo Loyd Nchunga.
Hata hivyo kumeibuka hali ya sintofahamu juu ya sababu zinazo pelekea TFF kushindwa kukamilisha uhakiki wao hii leo wakati vyeti vilivyo wasilishwa TFF na kamati ya uchaguzi ya Yanga kuwa vimeiridhisha katika kamati ya uchaguzi ya Yanga.
Akizungumza na Rockersports katibu wa kamati ya uchaguzi ya klabu ya Yanga Fransis Kaswahili amesema tatizo kubwa ni kutokana na kanuni za Yanga kutojitosheleza kimahitaji jambo ambalo limeifanya kamati ya Uchaguzi ya TFF kuendelea kuburuza Uchaguzi wa Yanga kiasi hiki.
Miongoni mwa wagombea ambao cheti chake pia kinahakikiwa ni pamoja na mgombea wa nafasi ya ujumbe Abdalah Bin kleb.
No comments:
Post a Comment