KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, August 12, 2012

MBUYI TWITE,KELVIN YONDANI NA ANGETILE OSEAH WAMUONDOA RAGE TFF.


 Mjumbe wa kamati ya sheria na katiba ya shirikisho la kandanda nchini TFF Ismail Aden Rage ambaye pia ni mwenyekiti wa mabingwa wa soka nchini Tanzania Simba, amaua kujizulu kutoka katoka katika kamati hiyo ya tff kufuatia sakata la usajili wa mlinzi wa APR ya Rwanda Mbuyi Twitte ambaye inaarifiwa kuwa amejiunga na klabu ya Yanga.
Sambamba na hilo pia Rage amefikia umauzi huo baada ya kubaini kuendelea kufanyika kwa madudu na mchezo mchafu unaofanywa na sekretarieti ya TFF ambayo imekuwa ikisimamia mambo bila kufuata kanuni na taratibu.
Akiongea na Rockersports Rage amesema kuna mambo mengi ambayo yamekuwa yakiamuliwa kwa kukidhi matakwa ya klabu Yanga hata kama ni kwa kuvunja sheria hasa panapo kuwepo na ‘conflict of interest’.
Rage amesema mara mbili amemuandia barua Rais wa TFF Leordigar Tenga juu ya madudu hayo lakini bado kumeendelea kujitokeza uvunjifu wa kanuni na sheria hasa katika kamati ya maadili na katiba ambako yeye pia mjumbe.
Amesema mara nyingi linapo jitokeza suala la kuijadili Simba ili kuruhusu haki kutendeka amekuwa akitoka nje ili kutoa nafasi kwa suala hilo kujadiliwa kwa uwazi na sheria kuchukua mkondo wake lakini hilo limekuwa halifanywi na viongozi wa vilabu vingine hasa Yanga na maamuzi kuwa ni ya upendeleo.
Jambo lingine Rage amesema ni kuridhika kwa Sekretarieti ya TFF juu ya mchezaji wake mlinzi wa Kelvin Yondani kutolewa kambini usiku mwingi kwa lengo la kukamilisha usajili katika klabu ya Yanga jambo ambalo amesema alimuandikia barua Rais Tenga kumuarifu juu ya hilo lakini kabla ya hatua kuchukuliwa kamati ndogo ya sheria ya TFF chini ya katibu wake Angetile Oseah iliamua kumuidhinisha Kelvin Yondani kuchezea Yanga katika michuano ya kombe la Kagame.
Rage pia amezungumzia juu ya usajili wa mlinzi wa kati wa APR ambaye kwasasa amesajiliwa na Yanga amesema kuna mkono wa TFF kwani hilo limethibtishwa na Rais wa klabu ya APR Meja Jenerali Alex Kagame pale alipozungumza naye juu ya taarifa za mabadiliko ya usajili wake kwenda Yanga.
Amenukuliwa Rage na Rockersports akisema
 “wakati taarifa hizo zilipotufikia  Simba niliamua  kumpigia simu Rais wa APR Meja Jenerali Alex Kagame ambaye alinithibtishia kuwa ni kweli klabu yake ilitoa ruhusa Simba kumchukua Mbuyi na si Yanga, lakini kilicho fanyika ni kuwa amepewa maagizo na wakubwa kumsainisha Twite katika klabu ya Yanga na hivyo taratibu za uhamisho zikafanyika ili mchezaji huyo ajiunge na Yanga”.
“nikiendelea kuzungumza naye alisema kuwa kuwa suala hilo limemfunga mikono kwani kuna maagizo kutoka juu na kwamba kuna motto wa kigogo aliyekuwa ana shughulikia suala hilo, hivyo lilikuwa juu ya uwezo wake”
Rage amewashukuru wajumbe wote aliokuwa nao katika kamati hiyo kwa ushirikiano wao na yeye ameamua kukaa pembeni lakini amemshukuru Rais Tenga kwa kumteu na kuwa na imani naye katika kipindi chote alichukuwepo ndani ya kamati hiyo.
Rage ameitahadharisha TFF na Serikali kuwa uvumilivu wa wanachama wa Simba utafika mwisho na wasipokuwa makini watahatarisha amani ya nchi kwani  huko nchini Kenya hivi karibuni  timu ya Abaluya na Gor Mahia wapenzi wao waliuana kwa mambo kama hayo ya michezo, hivyo tunapaswa kuwa makini.

1 comment:

  1. Simba na Rage kilichobaki ni kuendelea kulia tu ...

    ReplyDelete