Di Matteo: Bado
namtaka Ashley Cole asaliye Chelsea.
Meneja wa Chelsea
Roberto Di Matteo anataka mlinzi wake wa kushoto Ashley
Cole kusaini mkataba mpya na kusalia darajani wakati huu ambapo
kumekuwepo na taarifa kuwa Real Madrid na Paris Saint-Germain zimekuwa zikimkodolea
macho.
Mlinzi huyo
wa kushoto anatarajia kumaliza mkataba wake na 'The Blues' wakati wa kipindi cha majira ya
kiangazi, lakini akiwa bado ni miongoni mwa wachezaji walio katika mpango wa sera za mmiliki
wa klabu hiyo Roman Abramovich wa kuongezewa mkataba, mpango ambao ni wa nyongeza
ya mkataba wa mwaka mmoja kwa wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 30.
Taarifa zinasema
kuwa mpango huo ni wa kisera ambao ulimuondosha mshambuliaji wa Tembo wa
Ivory Coast Dider Drogba mwishoni mwa msimu uliopita.
Real Madrid
na Paris Saint-Germain wanaonekana kuwa tayari kupeleka pendekezo la awali
la kumtaka mlinzi huyo mwezi January na baadaye kukamilisha usajili wake, wakati mkataba wake
darajani utakapo malizika huku bodi ya Chelsea ikiwa na muda wa miezi miwili kufikiria
hilo na kulitolea maamuzi.
Akinukuliwa Di
Matteo amesema
"maoni
yangu na matarajio yangu ni Cole kusalia, lakini hatma yeke iko katika bodi ambayo
itakuwa na maamuzi ya mwisho juu ya hilo"
Nelspruit kujaa katika fainali za
mataifa ya Afrika.
Meneja wa
uwanja wa Mbombela uliopo Nelspruit Roelf Kotze, anaamini uwanja huo utawavutia
watu wengi katika fainali za mataifa ya Afrika zitakazo fanyika nchini Afrika
kusini mwakani.
Uwanja huo
unatarajiwa kuchezewa michezo minane ikiwepo michezo ya robo fainali na nusu
fainali.
Mchezo unaotazamiwa
kujaza watu wengi zaidi katika uwanja huo ni mchezo wa kundi C kati ya mabingwa
watetezi Zambia dhidi ya Nigeria Januari 25.
Amenukuliwa akisema,
"tunaimani
kuwa uwanja utakuwa na idadi kubwa ya watazamaji "
Michezo mingine
itakayo chezewa katika uwanja huo ni pamoja na
21/01/2013
Zambia v Ethiopia;
Nigeria v
Burkina Faso (Group C)
25/01/2013
Zambia v
Nigeria
Burkina Faso
v Ethiopia (Group C)
29/01/2013
Zambia v
Burkina Faso (Group C)
30/01/2013
Togo v
Tunisia (Group D)
Robo fainali
03/02/2013
Nusu fainali
06/012/2013
Amesema kuwa
hata hivyo kazi bado inatakiwa kufanyika ili kuhakikisha watu wanachomoza kwa
wingi kwani wastani wa mahudhurio katika uwanja huo ni watazamaji elfu 16 mpaka
17.
Pamoja na Nigeria
na Zambia, mji huo unatarajia kuwa mwenyeji wa timu za taifa za Burkina Faso,
Ethiopia, Togo na Tunisia.
Kotze ana
matumaini michezo hiyo itavutia watu wengine kutoka nje ya Nelspruit.
Wakati hayo
yakiwa hivyo, baraza la mawaziri nchini Afrika Kusini limeidhinisha fungu la
kiasi cha dolari za kimarekani milioni 52 kwa kamati ya maandalizi ya nchi hiyo(LOC).
Kiasi cha
dolari milioni 9.5 zitatumika kwa ajili ya gharama za uendeshaji na kiasi
kitakacho salia ni kwa ajili ya usimamizi mzima wa michuano katika miji mitano
itakayo kuwa wenyeji wakati wa michuano.
No comments:
Post a Comment