Rais wa
shirikisho la soka nchini Leordigar Tenga amewataka wadau wa soka nchini
kujitokeza kuichangia timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti
Boys wakati huu ambapo timu hiyo inajiandaa kwa ajili ya mchezo wao wa mzunguko
wa tatu dhidi ya ama Zimbabwe au Congo ambao wanatarajia kukutana hivi
karibuni.
Tenga
amesema mpaka hivi sasa timu hiyo haijapata mdhamnini na imekuwa ikiligharimu
shirikisho la soka nchini TFF pesa nyingi ambapo ni kwa ajili ya malazi,
chakula na posho za wachezaji wakati huu ambapo wamekuwa wakiendelea na mazoezi
yao.
Amesema mpaka sasa kikosi hicho cha timu ya Taifa ya vijana kimesha igharimu TFF kiasi cha shilingi za milioni 250 lakini pia kuna wadau kama NSSF, NMB, chama cha soka mkoa wa Mbeya na PPF ambao wamekuwa wakisaidia malazi yao na viposho vya wachezaji.
Tenga
amesema kocha mkuu wa kikosi hicho Jacob Michelsen ametaka kimsingi kuondoka
kwenda kutazama mchezo wa Zimbabwe na congo ili kujionea mwenyewe mbinu za
kiuchezaji za mpinzani wa Serengeti ambapo mpinzani akakuwa ni mshindi wa mchezo huo na
hivyo kupata fursa ya kukijenga kikosi hicho kabla ya mchezo wa mwisho wa
kukata tiketi ya kucheza fainali za vijana ambazo zinatarajiwa kuchezwa nchini
Morocco mapema mwakani.
Aidha
Michelsen ameomba apatiwe mchezo mmoja wa kujipima nguvu kabla ya mchezo huo wa
mzunguko wa tatu na tayari Botswana na Afrika kusini wameonyesha nia ya kutaka
kucheza na Serengeti Boys.
Tenga
amesema katika kufanikisha yote hayo kunaifanya TFF kuelemewa na mzigo wa
gharama ambazo zinatoka na usafiri wa timu itakayo kuja nchini kucheza mchezo
huo,malazi na chakula pamoja na waamuzi watakao chezesha mchezo huo.
Tenga
amesema ameona vema kuliweka hilo wazi ili kutoa nafasi kwa wapenzi wa mpira na
wadau wengine kujitokeza kuichangia timu hiyo kwa lengo la kutimiza azma
iliyokuwepo ya kujenga wachezaji vijana ambao watakuwa azina ya taifa.
WAKATI HUOHUO
Rais wa
shirikisho la soka nchini Sir Leodiger Chila Tenga amevitaka vilabu vya ligi
kuu chini ya kamati ya ligi pamoja na vyombo vya habari nchini kuketi meza moja
na kujadili juu ya mzozo uliobuka hivi karibuni, ambapo uongozi wa vilabu hivyo vilipiga
marufuku michezo ya ligi kuu kutokuonyeshwa moja kwa moja na televisheni wala
kutangazwa na redio kwa madai ya kutaka matangazo hayo kulipiwa na vyombo hivyo
vya habari.
Kauli ya
kupiga marufuku ilitolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa kamati ya ligi Wallece
Karia ambapo marufuku hiyo ilianza kuonekana katika mchezo wa ligi uliochezwa
jumamosi katika uwanja wa Taifa baina ya Simba na Mtibwa ambao ulimalizika kwa
Simba kuchomoza na ushindi wa mabao 3-1.
Kabla ya
kuanza kwa mchezo huo, walionekana walinzi wakiwazuia wanahabari kupiga picha
za mchezo huo na kupelekea matukio muhimu ya nje ya mchezo huo ukiwemo mchezo
wenyewe kutokurekodiwa wala kuripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari hapa
nchini.
Akiongea na
waandishi wa habari Rais Tenga amesema ameamua kulizungumza hili mapema kwa
lengo la kutolea ufafanuzi lakini pia kuzitaka pande zote mbili kuketi meza
moja na kulizungumza kwa lengo la kupata muafaka wa mzozo huo.
Amesema TFF
aliamua mambo ya undeshaji wa ligi kusimamiwa na viongozi wenyewe wa vilabu kwa
kushirikiana na kamati ya ligi na hivyo kwa kuwa mambo hayo yana ugumu wake
ndio maana viongozi hao wanahangaika kutafuta namna ya kuongeza vipato vya
wakati huu mchakato wa kuelekea kuundwa kwa bodi maalumu itakayokuwa na jukumu
la kuisimamia ligi hiyo.
Amesema yeye
kama Rais anajua umuhimu wa vyombo vya
habari katika kuutangaza mchezo wa soka na mchango mkubwa unao patikana kupitia
vyombo vya habari katika kuutangaza mchezo wa soka kote duniani.
Tenga
amesema ni kweli kote duniani vilabu vya soka huwa vinanufaika na vyombo vya
habari kupitia matangazo ya mpira lakini kwa hapa kwetu ili kufikia azma hiyo
ya kamati ya ligi na vilabu basi ni vema watu wakazungumza a kuona ni jinsi
gani wataongeza vipato vyao kama kamati wakati huu wa kuunda bodi lakini anaona
ni vema hili likazungumzwa kutona na kile anacvho amini juu ya umuhimu wa
media.
"Nataka watu wengi wasikie habari
za mpira na si nvema tukatengeneza mazingira ya watu kutokupata habari za mpira
."
‘Tumekaa na
watu wa ligi na tumewataka wakae na vyombo vya habari na wazungumze juu yahilo.’
No comments:
Post a Comment