KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 29, 2012

FUKUZA FUKUZA YA MAKOCHA AZAM FC YAENDELEA, BORIS BUNJAK aka BOCA NAYE ATIMULIWA.

 Taarifa zilizo ifikia Rockersports na kuthibitshwa na mmoja wa viongozi wa klabu ya Azam fc inayoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania Bara ni kwamba klabu hiyo imemfuta kazi kocha wake Boris Bunjak maarufu kama Boca aliyechukua mikoba ya Mwingereza Stewart John Hall aliyetimuliwa kazi mwezi tarehe 31/Julay/2012.

Boris ambaye aliajiriwa kazi August 7 ya mwaka huu ametimuliwa kazi ikiwa ni siku mbili zimepita baada ya Azam fc kupokea kichapo cha mabao 3-1 toka kwa mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu Simba mchezo uliofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Makamu mwenyekiti wa Azam Said Mohamed Said alimsainisha Boris mkataba wa miaka miwili huku kocha huyo akiondoka ndani ya viunga vya Chamazi katika kipindi cha miezi mitatu.
Chini ya Stewart Hall, Azam FC ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mapinduzi Cup, Kushika nafasi ya pili katika ligi kuu, Mashindano ya Urafiki na Kombe la kagame yakiwa ni mafaniko ambayo hayajawahi kufikiwa na makocha wote waliotangulia katika historia hiyo.
Wakati huu Boris akiondoka na akisakwa mrithi wake kwa sasa timu itakuwa chini ya fundi wa viungo Vivek Nagul na kocha msaidizi Kally Ongala.

No comments:

Post a Comment