Bosi wa
kikosi cha timu ya taifa ya Argentina Alejandro Sabella ametaja kikosi cha
wachezaji 23 kitakacho pambana na kikosi cha kocha Frank Rijkaard cha timu ya
taifa ya Saudi Arabia mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa katika mji wa Riyadh.
Lionel Messi,
Angel Di Maria, Javier Mascherano na Gonzalo Higuain wameendelea kuwemo katika
mpango ya bosi huyo lakini pia akiwajumuisha wachezaji wengine kadhaa wakiwa ni
sura mpya kabisa katika kikosi cha timu hiyo.
Nyota wa Wigan
Franco Di Santo ameingizwa kikosini
ikiwa ni mara ya kwanza kujumuishwa katika kikosi cha timu hiyo na amepata
nafasi hiyo baada ya kuonyesha uwezo katika michezo ya mapema ya kuanza msimu
wa ligi kuu ya England ‘Premier League season’.
Ricky
Alvarez wa Inter Milan ya Italia amejumuishwa akichukua nafasi ya Erik Lamela
wa Roma, wakati ambapo Fabian Rinaudo, Cristian Alvarez na Tino Costa kwa
pamoja wakijumuishwa kwa mara ya kwanza.
Baada ta
kushinda michezo ya kampeni ya kufuzu fainali ya kombe la dunia dhidi ya Uruguay
na Chile vijana hao watataka kushinda pia mchezo huu wa tatu mfululizo
kudhihirisha ubora wa kikosi chao.
Kikosi kizima
Walinda milango:
Sergio
Romero-Sampdoria
Mariano
Andujar-Catania
Cristian
Alvarez-Espanyol
Walinzi:
Hugo
Campagnaro -Napoli
Pablo
Zabaleta -Manchester City
Marcos Rojo-Sporting
Lisbon
Federico
Fernandez-Napoli
Ezequiel
Garay-Benfica
Luciano
Monzon-Lyon
Fabricio
Coloccini-Newcastle
viungo:
Fernando Gago-Valencia
Javier
Mascherano-Barcelona
Angel Di
Maria-Real Madrid
Augusto
Fernandez-Celta Vigo
Enzo Perez-Benfica
Tino Costa-Valencia
Ricky
Alvarez-Inter
Fabian
Rinaudo-Sporting Lisbon
washambuliaji:
Lionel Messi
-Barcelona
Sergio
Aguero-Manchester City
Gonzalo
Higuain-Real Madrid
Eduardo
Salvio-Benfica
Franco Di
Santo-Wigan
Sammer amekosea kwenda mbele ya jamii
kuikosoa Bayern, anasema Jens Lehmann.
Mlinda mlango
wa zamani wa kikosi cha timu ya Taifa ya Ujerumani Jens Lehmann amemkosoa mkufugenzi
wa michezo wa Bayern Munich Matthias Sammer kufuatia maoni yake ya hivi
karibuni kuwa amehuzunishwa na kiwango duni kinachoonyeshwa na wachezaji wa
timu hiyo.
Sammer ametoa
kauli ya kuonyesha kutokupendezwa na kiwango cha hovyo kinachoonyeshwa na
mabingwa wa Bundesliga kutokana na kichapo kutoka kwa BATE Borisov katika ligi
ya mabingwa Ulaya licha ya ushindi wao dhidi ya Werder Bremen, na Lehmann
anaamini kuwa nyota huyo wa zamani wa Borussia Dortmund ameenda mbali sana.
"sidhani
kama atakurupuka na kuzungumza juu ya kiwango cha Bayern katika vyombo vya
habari tena.
Hata hivyo
nyota huyo wa kimataifa wa zamani wa ujerumani akaenda mbele zaidi kwa kusema
maoni ya Sammer yana haribu taswira ya klabu
"hakutakiwa
kwenda kusema kitu kama hiki mbele ya umma kwasababu kufanya hivyo ni
kumaanisha Bayern imepoteza heshima yake”
David Villa: Nataka namba ya kudumu Barca lakini.....
David Villa ana
matumaini makubwa ya kupata muda mwingi wa kucheza katika klabu yake ya Barcelona,
lakini pia anakubali hilo si jambo rahisi kwa kuwa anakabiliwa na ushindani
mkubwa wa kupata namba katika kikosi cha kwanza ndani ya klabu hiyo.
Villa mwenye
umri wa miaka 30 alikuwepo katika kikosi kilicho anza jumanne ya jana ambapo
Barca uliibuka na ushindi wa mabao 3-0 mchezo wa Copa del Rey dhidi ya Alaves, na
alifanikiwa kufunga goli safi ambalo lilimrejesha katika matumaini zaidi.
"kama
ilivyo kwa mcheza soka yoyote nataka kucheza mara nyingi kwa kadri ya uwezo
wangu wote,".
"nacheza
katika klabu bora duniani na changamoto ya kupata namba ni kubwa. tunacheza
michezo mingi na kuna mashindano mengi.
Barcelona itarejea
katika ligi kuu jumamosi ambapo watakuwa wenyeji wa Celta Vigo.
No comments:
Post a Comment