Simon Msuva (kulia)
akijaribu kumpiga chenga beki wa JKT Mgambo Salum Kipanga.
|
Nadir Haroub Kanavaro akifurahia bao lake la kwanza katika mchezo wa ushindi kwa Yanga wa mabao 3-0. |
Mbuyu Twite akimpaka upako Kanavaro baada ya kufunga bao la kwanza katika mchezo dhidi ya Mgambo JKT. |
Mshambuliaji wa Yanga Didier Kavumbaguakijaribu kumtoka mlinzi wa Mgambo. |
Ligi kuu ya soka Tanzania Bara imeendelea tena hii leo kwa michezo minne kuchezwa katiika viwanja vinne tofauti hapa nchini.
Katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Yanga walikuwa wenyeji wa JKT Mgambo mchezo ambao umemalizika kwa Yanga kupata ushindi wa mabao 3-0 huku mabao yakifungwa Nadir Haroub Kanavaro akifunga bao la kwanza kwa kichwa baada ya mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na kiungo Athumani Iddi Chuji.
Bao la pili lilifungwa na Didier Kavumbagu kufuatia pasi safi ya Hamisi Diego Kiiza na bao la tatu likifungwa na Jerson Tegete baada ya kupokea mpira mrefu wa mlinzi wa pembeni Oscar Joshua.
Matokeo hayo yameifanya Yanga kufikisha alama 23 sawa na kinara wa ligi hiyo Simba ambaye alikuwa akiongoza ligi hiyo kwa muda mrefu tangu kuanza kwa ligi.
Wao Simba wakiwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro wamekwenda sare ya bao 1-1 na polisi ya huko matokeo ambayo yamewasononesha mashabiki wa Simba ambao walikuwa wakihitaji ushindi na timu ambayo imekuwa kibonde katika ligi na ambayo haijawahi kushinda hata mchezo mmoja tangu kuanza kwa ligi.
Matokeo hayo yanaifanya Simba iendelee kuongoza ligi kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ambapo Simba ina mabao 20 ya kufunga huku ikifungwa jumla ya mabao 8 na hivyo ikiwa na uwiano wa mabao 12( goal difference 12), ambapo Yanga ina mabao ya kufunga 21 huku ikiwa imefungwa mabao 10 ambapo itakuwa na uwiano wa mabao 11(goal difference 11)
(Tazama msimamo kulia)
Matokeo hayo yanaifanya Simba iendelee kuongoza ligi kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ambapo Simba ina mabao 20 ya kufunga huku ikifungwa jumla ya mabao 8 na hivyo ikiwa na uwiano wa mabao 12( goal difference 12), ambapo Yanga ina mabao ya kufunga 21 huku ikiwa imefungwa mabao 10 ambapo itakuwa na uwiano wa mabao 11(goal difference 11)
(Tazama msimamo kulia)
Kikosi cha Simba |
Mchezo mwingine ulikuwa ukichezwa katika uwanja wa Chamazi Complex ambapo Afrikan Lyon ilikuwa mwenyeji wa JKT Ruvu na matokeo ya mchezo huo ni kwamba JKT Ruvu imeichapa Lyon kwa mabao 4-2.
Mtibwa Sugar wakiwa katika uwanja wao wa Manungu imefanikiwa kuichapa JKT Oljoro ya Arusha mabao 2-1.
Ratiba michezo ijayo
Kesho.
Azam vs Coast Union (Chamazi Complex)
Toto Afrikans vs Kagera Sugar (CCM Kirumba Mwanza)
Mzunguko wa 12
NO | DATE | No. | HOME TEAM | AWAY TEAM | STADIUM | VENUE |
12 | 03.11.2012. | 82 | RUVU SHOOTING | TOTO AFRICANS | MABATINI | PWANI |
03.11.2012. | 78 | AFRICAN LYON | MGAMBO JKT | AZAM COMPLEX | DAR ES SALAAM | |
07.11.2012. | 79 | MTIBWA SUGAR | JKT RUVU | MANUNGU | MOROGORO | |
03.11.2012. | 81 | KAGERA SUGAR | TANZANIA PRISONS | KAITABA | KAGERA | |
03.10.2012. | 80 | YOUNG AFRICANS | SIMBA | NATIONAL STADIUM | DAR ES SALAAM | |
07.11.2012. | 83 | AZAM | JKT OLJORO | AZAM COMPLEX | DAR ES SALAAM | |
07.11.2012. | 84 | COASTAL UNION | POLISI MOROGORO | MKWAKWANI | TANGA | |
No comments:
Post a Comment