Waswahili husema
ngoma ya kitoto haikeshi, nautumia msemo huu hii leo baada ya washambuliaji wa Chelsea
usiku wa kuamkia hii kuwazidi maarifa walinzi chipukizi wa mzee Alex Ferguson
na hatimaye Chelsea kufanikiwa kutinga katika hatua ya timu nane za mwisho katika
michuano ya kuwania taji la Capital One na sasa wakiwasubiri Leeds United.
Chelsea ilifanya
makosa mawili ya kiulinzi ambapo United kupitia kwa mkongwe Ryan Giggs na Javier
Hernandez walifanikiwa kupata mabao ilhali Chelsea walipata bao la kwanza kwa
njia ya penati likifungwa na David Luiz .
Gary Cahill aliandika
bao la pili na kuifanya matokeo kusomeka 2-2 lakini Luis Nani akaandika bao la
tatu ambalo pengine ilidhaniwa Chelsea amelala katika mchezo huo, lakini jitihada
za vijana wa darajani zilizaa matunda baada ya kufanikiwa kupata penati
iliyopigwa na Eden Hazard na matokeo kusomeka 3-3.
Daniel
Sturridge na Ramires kila mmoja alifunga goli katika dakika za nyongeza kabla
ya Rayan Giggs kufunga bao la penati ambalo liliufanya mchezo huo kumalizika
kwa matokeo ya Chelsea ikishinda 5-4.
Hatua ya
robo fainali itakuwa kama hivi,
Bradford v Arsenal
Leeds
United v Chelsea
Norwich
City v Aston Villa
Swansea
v Middlesbrough
Hata hivyo Chelsea
itabidi wamshukuru mlinzi wa kati chipukizi Scott Wootton, ambaye alimsukuma Ramires
na hivyo Chelsea kuzawadiwa penati katika dakika za nyongeza na mpira mwingine
wa kichwa cha kurudisha kwa mlinda mlango Anders Lindegaard kuwa mfupi na hivyo
kunaswa na Sturridge aliye utumbukiza nyavuni.
No comments:
Post a Comment