KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, October 14, 2012

AKINA DROGBA, YAYA NA KOLO TOURE WAOKOLEWA NA POLISI HUKO SENEGAL. MCHEZO WA SENEGAL NA IVORY COAST KUWANIA KUFUZU MATAIFA YA AFRIKA WAVUNJIKA BAADA YA MASHABIKI WA SENEGAL KUANZISHA VARANGATI NA MAJANGA DAKIKA ZA MWISHO MWISHO.



Mchezo mkubwa wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika baina ya Senegal na Ivory Coast umevunjika hapo jana baada ya mashabiki wa soka wa timu ya taifa ya Senegal kuanzisha vurugu kubwa uwanjani mjini Dakar.
Mashabiki hao walianza kuwasha moto vitu mbalimbali na kurusha vitu uwanjani wakati wakielekea kuupoteza mchezo huo kufuatia kuwa nyuma kimatokeo kwa bao 2-0 matokeo ambayo kimsingi yalikuwa yanaiondoa Senegal mashindanoni.
Wakati hali ya mambo ilivyozidi kuwa mbaya mashabiki wa Ivory Coast walilazimika kukimbilia uwanjani kuokoa maisha yao.
Mashabiki na wachezaji wa Ivory Coast walilazimika kusindikizwa na pilisi ambao walikuwa wakifyatua mabomu ya machozi kuelekea majukwaani.
Mashabiki walikuwa wakirusha vitu pamoja na kuchana bendera za taifa lao na kupelekea mambo kuwa shaghala bagala

Taarifa zinasema watu 10 akiwemo waziri wa michezo wa Senegal Hadji Malick Gakou wamejeruhiwa kutokana na ghasia hizo zilizo tokea katika uwanja wa Leopold Sedar Senghor.
Ghasia hizo zilianzia pale mshambuliaji wa tembo wa Ivory Coast Didier Drogba alipofunga goli kwa njia ya penati zikiwa zimesalia dakika 15 mchezo huo kumalizika.
Matokeo hayo yalikuwa yanawaondosha Senegal kwa kufungwa magoli ya jumla 6-2 baada ya michezo miwili ya nyumbani na ugenini.
Taarifa zaidi zinasema vurugu hizo ziliendelea zaidi hata katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dakar.
Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) bado halija toa tamko lolote kuhusiana na tukio hilo.
Lakini maafisa wa soka nchini humo wamenukuliwa wakisema CAF itatoa adhabu yake kwa nchi hiyo.
Ndugu wawili toka klabu kubwa nchini Uingereza ya Manchester City Yaya na Kolo Toure walikuwa ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Ivory Coast lakini wote wamesalimika

No comments:

Post a Comment