KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, October 14, 2012

LAMPARD NA BERTRAND NJE KIKOSI CHA ENGLAND, XAVI ANASEMA MESSI SHAURI NYINGINE ASIFANANISHWE NA RONALDO, ROBINHO ANASEMA KAMA ALLEGRI ANA HATIA BASI NA WACHEZAJI HIVYO HIVYO NA LUCAS ANAOTA MATAJI LIVERPOOL.


Chama cha soka ncini England FA kimethibitisha kuwa wachezaji wawili wa Chelsea Frank Lampard na Ryan Bertrand hawatakuwemp katika kikosi cha nchi hiyo katika mchezo wa kuwania nafasi ya kushiriki fainali ya kombe la dunia 2014 dhidi ya Poland mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa jumann e kutokana na kusumbuliwa na majeraha na kuumwa.
 
Taarifa ya FA imenukuliwa ikisema,
"Frank Lampard na Ryan Bertrand wameondolewa katika kikosi cha England kwa ajili ya mchezo wa kuwani kufuzu kombe la dunia dhidi ya Poland,"

"Lampard ana matatizo ya msuli na Bertrand ni mgonjwa ndio maana hawakuwepo katika kikosi kilichopata ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya San Marino, na pia hawatakuwepo katika mchezo wa jumanne"

Meneja Roy Hodgson hapo kabla alikuwa akimtegemea Lampard kwamba huenda kapata nafuu na kuwepo katika mchezo huo utakao pigwa kule Warsaw.

Xavi amsifia Messi kwa kusema hakuna kama Messi
Nyota wa Barcelona Xavi amemsifia nyota mwenzake katika timu yake ya Barcelona Lionel Messi, kwa kusema hakuna kama yeye,  akiwazodoa wanao mfananisha na Cristiano Ronaldo lakini pia akimpa heshima kocha wake Tito Vilanova, kwa kusema ana mambo mengi yanayo fanana na mtangulizi wake Pep Guardiola.

Amenukuliwa na rediao Catalunya akisema,
"ndani ya chumba cha kubadilishia nguo, ‘Leo’ Messi ni mtu mmoja mkimya sana. Ni mtu wa kipekee"
  "ni namba moja kwa upande wangu hakuna mwingine. Kwa kusema haki ni bora kabisa, na mchezo wake ni muhimu na bora kuliko Cristiano [Ronaldo]."

Xavi na Messi wamekuwa msaada mkubwa kwa Barcelona na kupelekea kutokupoteza mchezo katika ligi kuu ya soka nchini Hispania ‘La Liga’ ndani ya michezo saba wakiwa na kocha mpya Vilanova, ambaye anafuata nyayo za Guardiola na kupelekea klabu hiyo kupata matokeo mazuri.

Ameendelea kunukuliwa Xavi akisema
"Pep na Tito, wanatofauti ndogo sana ya kiufundi, ni kama wana fanana. Guardiola alikuwa anapenda vitendo, na Vilanova hayuko mbali "
 "Tito amekuwa akinishangaza, kwasababu anaonekana kujiandaa sana, akiwa na mawazo yaliyo wazi na anaendeleza ‘philosophy’ ya klabu.

Robinho amtetea bosi wake Allegri
Mshambuliaji wa AC Milan Robinho amemtetea kocha wake ambaye yuko katika hali tete juu ya kibarua chake Massimiliano Allegri, akisisitiza kuwa wachezaji wako nyuma yake.

Rossoneri imeshinda michezo mitatu katika michezo mbalimbali ya kimashindano mpaka sasa msimu huu huku hatma ya Allegr ikiingia mashakani tangu kichapo cha bao 1-0 toka kwa wapinzani wao wakubwa Inter Milan katika ile inayotambulika kama ‘Derby della Madonnina’ wiki iliyopita.

Akinukuliwa na Gazzetta dello Sport Robinho amesema,
"Ni ngumu na msimu hauwezi kuwa umeanza mpaka timu ishinde, Kama Allegri yuko katika matatizo hata sisi ni hivyo. Lakini mpira wa miguu unatufundisha kuwa mambo yanaweza badilika haraka"
"inachukua michezo miwili mpaka mitatu unacheza vizuri lakini baadaye unarudi kule kule. 

Mchezo na Inter, walistahili kushinda lakini hii aibu baada ya kichapo tu, presha imepanda zaidi.

"haya mambo ni ya kawaida. Najisikia vibaya kumuona Allegri anaingia katika kipindi kigumu kama hivi na minong’ono mingi dhidi yake.

 Lucas bado anajipa moyo na mataji Liverpool
Lucas Leiva anaamini kuwa Liverpool inaweza kubadilika na kutoa changamoto mpya katika kutwaa mataji ya ligi kuu ya nchini England ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo hususani baada ya klabu hiyo kumuajiri Brendan Rodgers na wachezaji muhimu kuongeza mikataba.

Wekundu hao wameshindwa kufuzu klabu bingwa ulaya kwa kipindi cha miaka mitatu sasa, baada ya matokeo mabovu ya michezo ya ligi , lakini meneja mpya aliye ajiriwa katika kipindi cha majira ya kiangazi akitokea Swansea Rodgers ameanza kujenga upya kikosi cha klabu hiyo.

Kitendo cha kusaini upya mikataba yao kwa wachezaji kama Luis Suarez, Daniel Agger na Martin Skrtel kunampa imani Lucas mwenye umri wa miaka 25 kuamini Liverpool ina kikosi ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mambo ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Amenukuliwa akisema,
"ndani ya kipindi cha miaka mitano, nina imani kuwa tunaweza kushinda taji la ligi na klabu bingwa ulaya. Kwanini isiwezekane? Tunapaswa kuamini hivyo. Hii klabu inaonyesha wazi kuwa tunaweza kwanini tusirejee katika enzi zile ?"

No comments:

Post a Comment