KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 15, 2012

Meneja wa timu ya taifa ya Senegal anasema watakubali adhabu.


Meneja wa timu ya taifa ya Senegal Ferdinand Coly amesema wanatarajia kuwa katika kipindi kigumu mbeleni, baada ya vurugu zilizo sababishwa na mashabiki wa soka wa nchi yao kiasi kupelekea mchezo wa kuwania kufuzu fainali za maraifa ya Afrika dhidi ya Ivory Coast  kuvunjika jumamosi.
 
Vurugu hizo zilitokea wakati ambapoa Ivory Coast ikiongoza kwa mabao 2-0 ambayo yalikuwa ni matokeo ya jumla ya mabao 6-2.

Amenukuliwa Coly akisema
"tunaelekea katika wakati mgumu lakini Senegal itakubaliana na adhabu".

"kwa wachezaji imewaumiza sana hususani wachezaji wachanga"
Mashabiki wa Senegal walianza kuwasha moto majukwaani na kutupa vitu uwanjani zikiwa zimesalia dakika 15 mchezo huo kumalizika mjini Dakar, muda mfupi baada ya mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba kukandamiza bao la pili kwa njia ya penati.

No comments:

Post a Comment