NITAIVUNJA RIKODI YA SIR CHARLTON YA KUPASIA NYAVU MAN UNITED NA TIMU YA TAIFA
Wayne Rooney
amedhamiria kuivunja rekodi ya ufungaji iliyowekwa na Sir Bobby Charlton katika
klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 27 kwasasa yuko katika nafasi ya nne ya wafungaji
bora waliowahi kupita United akiwa ameshafumania nyavu mara 185 ambayo ni
pungufu ya mabao 64 ya Charlton ambaye anaendelea kushikilia rekodi ya ufungaji
ya klabu hiyo ya mabao 249.
Katika timu
ya taifa ya England ‘Three Lions Rooney’ Rooney amefunga jumla ya magoli 32 ambayo
ni pungufu mabao 17 kufikia rekodi ya Charlton ya mabao 49.
Amekaririwa Rooney
akisema
"Sir
Bobby anashikilia rekodi zote mbili, hii
ni changamoto kubwa sana, jamaa ni mwasisi katika klabu kwahiyo ni kama mtu
ambaye anaendelea kuwepo katika klabu, kama nitafanikiwa kuvunja rekodi yake ya
ufungaji bora katika klabu na hata katika timu ya taifa hilo litakuwa ji jambo la
kupendeza."
Rooney pia
anataka kucheza soka katika kipindi kirefu zaidi kama ilivyo kwa Ryan Giggs na Paul
Scholes wachezaji ambao wanamvutia kwa kuendelea kuwepo kwa zaidi ya muongo
mmoja.
Nahodha wa Chelsea Terry nje kwa wiki
tatu
Meneja wa Chelsea
Roberto Di Matteo amethibitisha kuwa John Terry atakuwa nje ya uwanja kwa
takribani wiki tatu kufuatia kuwa majeruhi wa mguu.
Kuna wasiwasi
kuwa huenda mlinzi huyo wa kati akaendelea kuwa nje kwa kipindi kirefu zaidi
kutokana na kuwepo taarifa kuwa mguu wake ambao aligongana na mshambuliaji wa
Liverpool Luis Suarez katika mchezo wa jumapili uliomalizika kwa sare ya bao
1-1, kupinda kidogo.
Mlinzi huyo
wa kimataifa wa England alionekana akigumia kwa nguvu kutokana na maumivu na
kisha kutolewa nje kwa kutumia machela katika dimba la Stamford Bridge ambapo kipimo cha 'MRI scans' hapo kabla
kikonyesha alipatwa na madhara kidogo katika mshipa wa mguu.
Hata hivyo bosi
wa ‘The Blues' Di Mateo ametanabaisha kuwa mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 31
atakosekana kwa wiki tatu jambo ambapo amesema ni pigo kwa kikosi chake.
Dante: Nimekuja Bayern kusaka mataji
na si kuuza sura
Mlinzi wa
kati wa Bayern Munich Dante amesema waziwazi kuwa kilichomshawishi kujiunga na
klabu hiyo si kingine isipokuwa anahitaji kushinda mataji.
Mlinzi huyo
wa zamani wa Borussia Monchengladbach alijiunga na Bavaria kwa ada ya euro million
4.7 katika kipindi cha uhamisho wa kiangazi baada ya kuipa mafanikio Gladbach
katika msimu wa 2011-12 ambapo ilimaliza katika nafasi ya nne katika msimamo wa
ligi ngumu kabisa ya nchini Ujerumani ‘Bundesliga’.
Akiwa hajawahi
kushinda taji lolote kubwa katika soka , mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 29
anafikiria ndoto yake itatimia kwa kujiunga na kikosi cha kocha Jupp Heynckes.
Beckham hana mpango wa kuondoka LA
Galaxy na kuelekea Australia
Msemaji wa Kiungo na nahodha wa zamani wa England David Beckham amekanusha taarifa kuwa mchezaji huyo ana mpango
wa kuihama klabu yake ya LA Galaxy na kuelekea nchini Australia baada ya
shirikisho la soka nchini Australia (FFA) kudai kuwa kiungo huyo ambaye kwasasa
ana umri wa miaka 37 alikuwa anaitamani ligi kuu ya soka ya nchi hiyo ya A-League.
Msemaji wa FFA
amedokeza kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United alikuwa katika
mpango wa kufuata nyayo za akina Alessandro Del Piero na Emile Heskey na
kujiunga na soka la Australia.
Taarifa kupitia
msemaji wa FFA ambazo zilionyesha ni kama kuifagilia ligi ya Australia
imesomeka
"kuja
kwa David Beckham ni ishara kuwa hadhi ya ligi yetu ya Hyundai A-League imekuwa
duniani.
"Beckham
ni nyota mkubwa sana duniani na atakuwa mtu mwingine mkubwa katika soka
kujiunga na Hyundai A-League baada ya kuja kwa Alessandro Del Piero, Emile
Heskey na Shinji Ono. Lakini kwasasa ujio wake bado uko katika hatua za awali"
Hata hivyo
msemaji wa Beckham amekanusha taarifa hizo akisema mchezaji huyo kwasasa ana
furahia maisha katika jiji la Los Angeles na hana mpango wa kuondoka.
No comments:
Post a Comment