KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, November 17, 2012

CHAKULA CHA JIONI KWA SERENGETI JB BELMONTE: NENO KUBWA NI KUPIGANA NA VIJEBA WA CONGO BRAZZAVILLE MPAKA KIELEWEKE.

Meza kuu kutoka kushoto ni mama Juliana Matagi Yasoda, Rais wa TFF leodigar Tenga na Kassim Dewji.
Kocha mkuu wa Serengeti Boys Jacob Michelsen na msaidizi wake Jamhuri Kihwelu.
Vijana wa Serengeti katika maakuli ya jioni.
Mzee Said Mohamed katikati katika meza moja Wallece Karia.
Henri Tandau ambaye ni mjumbe wa kamati ya Serengeti hapa alikuwa mshereheshaji.
Waandishi wa habari Vicki Kimaro na Tullo Chambo.
Mayemba
Nassor na Dewji.
Wadau mbalimbali.
Ahaji Mgoyi na Kassim
Waandishi Amri Msare wa Capital Radio na Deogratius Mnyonga wa jambo Leo.
Dereva wa basi la vijana wa Serengeti Haji akinga menu na kijana wake.
Omar Katanga.
Wachezaji wa Serengeti.
Wajumbe wa kamati ya Serengeti Abdalah Bin Kleb akiwa SalimSeif.
Nahodha wa Serengeti Miraji Adam mwenye kipaza sauti akiwa na Hussein Twaha anayepiga makofi.
Timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys usiku wa jana ilifanyiwa hafla fupi ya chakula cha jioni kilicho andaliwa na kamati maalumu ya kuhamasisha watanzania kuichangia timu hiyo pamoja kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika mchezo wake dhidi ya timu ya vijana kutoka Congo Brazzavalle hafla ambayo ilifanyika katika hoteli ya JB Belmonte iliyo katika ya jiji la Dar es Salaam.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali kwa lengo la kubadilishana mawazo, pamoja na kutunisha mfuko wa Serengeti ambao inahitaji shilingi milioni 162 ili kufanikisha azma ya kutinga fainali za mataifa ya Afrika, fainali ambazo zitafanyika mwakani nchini Morroco.

Rais wa shirikisho la soka nchini Leodigar Tenga alipata nafasi ya kusema yake machache ambapo alirejea wito wake wa kuwataka vijana hao kuhakikisha wanafanya vizuri kwa kutekeleza maagizo ya makocha wao Jacob Michelsen na Jamhuri Kihwelu huku wakijua wazi kuwa wamebeba roho za watanzania wengi nyuma yao ambao wanawaunga mkono.

Amewata kuiga mfano wake ambapo mbali ya kuichezea timu ya Taifa katika miaka ya sabini na themanini lakini pia alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ambayo ilishiriki kwa mara ya mwisho fainali za mataifa ya Afrika.

Amewataka pia kukumbukua maneno mazuri aliyozungumza gwiji la zamani la soka barani Afrika Abeid Pele ambaye alikuwepo nchini hivi karibuni ambapo mmoja wa wachezaji wa Serengeti Husein Twaha alimnukuu Pele alipozungumza nao uwanja wa Karume pale alipowatembelea maneno ambayo hyaliwasisimua wadau waliokuwepo ukumbini hapo.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati ya Serengeti Kassim Dewji amewataka vijana hao kusahau maneno ya kuwa Congo imekuja na wachezaji vijeba na badala yake wafanyekazi kuhakikisha wanawadhibiti vilivyo na ushindi upatikane.

Dewji amesema yeye anaamini maandalizi waliyofanya vijana hao ni mazuri na kwamba wahakikishe wanachomoka na ushindi wa kishondo katika mchezo wa jumapili ili kuwapa kazi ya ziada katika mchezo wa marudiano utakao fanyika nchini Congo wiki mbili baadaye.

Neno zuri kwa vijana hao kutoka kwa Dewji ni kwamba anaamini watavuka hatua hiyo na wataelekea Morroco Mwakani na kwamba baada ya fainali za Morroco basi mungu akipenda wachezaji zaidi ya 15 watape timu za kucheza barani Ulaya.

Naye mwenyekiti wa Azam mzee Said Mohamed alikumbushia namna alivyocheza soka wakati wa ujana wake ambapo alisema alikuwa hodari katika kupenyeza mipira ya krosi ambapo alikuwa na uwezo wa kukimbia na kupiga jambo ambalo lilikuwa likimfurahisha kocha wake na hivyo vijana hao waige mfano wake.

Nassor Bin Slum akiwawakisha wajumbe wenzake wa kamati amewataka vijana hao kuhakikisha wanafanya vizuri kama ambavyo wajumbe wengine walivyosema.

Mama Juliana Matagi Yasoda akiwa ni mwakilishi wa serikali toka kurugenzi ya michezo wizara ya habari utamaduni na michezo amesema serikali iko nyuma ya vijana hao na kwamba imemshangaza kuona timu ya taifa ya vijana ikifanyiwa hafla nzuri kama hiyo jambo ambalo hakuwahi kuliona siku za nyuma.

Hata hivyo kilio chake ni kwamba wajitume kwa kadri wawezavyo na kwamba serikali inawasapoti.

Jacob na Kihwelu wamewahamasisha vijana kufanyia kazi yale wanayo wafundisha na kwamba wanaimani uwezo mkubwa wa kuwafunga Congo wanao.

Jamhuri Kihwelu amesema   kama wanataka kupata mafanikio na maisha mazuri katika maisha yao, basi muda sasa umefika wa kufanya hivyo ambapo endapo watawafunga wakongo basi kila mtu atajitokeza kuwachangia zaidi tofauti la ilivyo sasa.

Timu hiyo ya vijana imehashia kambi yake katika hoteli ya JB Belmonte na itaendelea kuwepo hapo mpaka baada ya mchezo wao dhidi ya Congo Brazzaville mchezo ambao utachezwa jumapili katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment