Ikiwa ni siku moja tu imepita baada ya baraza la wazee wa klabu ya Simba kuwataka wanachana wa klabu hiyo kuachana na mkutano uliotishwa na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo tarehe 30 desemba kwa madai kuwa mkutano huo si halali, hii leo kundi hilo limekutana na waandishi wa habari na kuendelea kusisitiza juu ya kufanyika kwa mkutano huo katika hoteli ya Travetine tarehe hiyo ambayo itakuwa ni Jumapili.
Jana akiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi za makao makuu ya klabu hiyo zilizopo Mtaa
wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es
Salaam jana, Kaimu Katibu wa Baraza la Wazee wa Simba, Zubery Mpacha, alisema
mkutano ulioitishwa (Jumapili) ni batili kwa sababu haujaandaliwa kwa kufuata
katiba ya klabu hiyo.
Mpacha
ambaye aliambatana na mwenyekiti wa baraza hilo, Hamis Kilomoni, na pia wajumbe wengine
wakiwamo Salehe Ally, Mzee Mkopi, Hamis Jongo na Juma Bulongo, alisema kuwa
katiba ya Simba hairuhusu wanachama kuandaa mkutano wa klabu bila idhini ya
uongozi.
Akijibu mapigo hayo hii leo mbele ya waandishi wa habari niaba ya wanachama wenzake wanaodaiwa kufikia 698, mwakilishi wa wanachama hao mzee Ally Mselem amesema mkutano wao uliopangwa kufanyika tarehe 30 mwezi huu uko palepale na amewataka wanachama wote wa Simba wenye uchungu na klabu yao kufika katika mkutano wao kwa kuwa katiba inawalinda.
Mselem ambaye alitumia muda mwingi kuuponda uongozi wa sasa ulioko madarakani chini ya mwenyekiti Ismail Aden Rage kuwa unalengo la kuishusha daraja Simba kwa kuwa viongozi wa sasa wameshindwa kuiongoza klabu hiyo.
Mselem pia alitumia maneno makali akiyaelekeza kwa mwenyekiti Rage ambaye alitamka kuwa mkutano huo si halali labda uwe ni kikao cha harusi.
Ameshangaa pia wazee wa klabu hiyo ambao jana waliwatangazia umma wa wana Simba kuwa mkutano wa tarehe 30 si halali ambapo Mselem amesema wazee hao wa Simba waliotoa kauli hiyo wanalinda maslahi yao.
Pia ameelezea historia ndefu ya uongozi wa Rage katika mpira huku akifafanya kila eneo ambalo mwenyekiti huo wa Simba aliongoza na kushindwa.
Maneno mengine magumu, sikiliza mwenye chini.
MZEE ALLY MSELEMU ANG'KA NA RAGE
BOFYA CHINI KUSIKILIZA.
No comments:
Post a Comment