Shinji
Kagawa anatarajiwa kuwepo katika benchi la Manchester United Jumamosi katika
mchezo dhidi ya West Brom.
Kiungo aliyejiunga
na United akitokea Borussia Dortmund alikuwa nje ya uwanja tangu October 23 kutokana na
kusumbuliwa na maumivu ya mguu mbayo aliyatapata katika mchezo wa vilabu bingwa
ulaya(champions league) dhidi ya Braga.
Hapo kabla alitarajiwa kuwepo
nje ya uwanja kwa wiki nne lakini kutokana na maumivu yeke kuendelea,
akalazimika kuendelea kuuguza mguu kwa siku zaidi na tangu wakati huyo
hajashuka dimbani.
Wakati hali
ya mambo ikiwa hivyo, meneja Sir Alex Ferguson amesema kwakuwa mambo yanakwenda
sawa kwasasa, anatarajia kuwa naye katika benchi jumamosi dhidi katika mchezo West
Brom.
Mzee ferguson
ameweka wazi kuwa anatarajia pia kuwa na Danny Welbeck pamoja naye Ashley Young
hiyo jumamosi licha ya kwamba hakuwa tayari kuthibitisha kama Wayne Rooney atakuwepo
ama la kama ilivyo kwa mlinzi Phil Jones ambaye ni dhihri shahiri atakosekana
hiyo kesho.
Birmingham yathibitisha Liverpool kumtaka mlinda mlango wao Butland.
Kaimu
mwenyekiti wa Birmingham City Peter Pannu amethibitisha kuwa Liverpool iko
katika mazungumzo na mlinda mlango Jack Butland.
Mlinda mlango
hivi karibuni aliarifiwa kuwa anatakiwa na Liverpool ambayo inataka kupata mlinda mlango mbadala wa Pepe
Reina.
Wakati huu
ambapo Birmingham inayoshiriki ligi ya pili ya England ya Championship ikiwa katika
hali mbaya kifedha tangu kushuka daraja kutoka ligi kuu “Premier League”, taarifa
zinasema kuwa klabu hiyo inahangaika kusaka pesa kwa kuuza baadhi ya wachezaji
wake wenye thamani ili kuweza kujinusuru na ukata huo.
Kaimu huyo
wa mwenyekiti wa St. Andrews, Pannu, amepangusa aibu ya kuingiliwa na ukata na anathibitisha waziwazi kuwa jogoo
wa England Liverpool ameonyesha nia ya kumtaka mlinda mlango wao kinda Butland na huenda akauzwa kujaribu kupunguza makali ya ukata na kusema kuwa ni Liverpool
pekee ambayo imeonyesha nia mpaka sasa kumtaka mlinda mlango huyo wa kimataifa
wa England.
Adhabu ya Meireles yapunguzwa mechi
nne licha ya kumchafua kwa mate usoni mwamuzi.
Kiungo wa Fenerbahce Raul Meireles amepunguziwa adhabu yake kutoka kusimama kwa michezo 11 na sasa kusaliwa na adhabu ya kusimama michezo 7 punguzo ambalo limefanywa na
shirikisho la soka la Uturuki( Turkish Football Federation (TFF)) .
Kiungo huyo
mreno mwenye umri wa miaka 29 hapo awali alipigwa adhabu ya kusimama michezo 11
kufuatia kushutumiwa kwa kosa la kumtea mate mwamuzi usoni baada ya mwamuzi
huyo kumlima kadi nyekundu katika mchezo ambao Fenerbahce walipata kibano cha
mabao 2-1 kutoka kwa Galatasaray.
Hata hivyo Meireles alikata rufaa ya kupinga adhabu hiyo na baadaye TFF iliona kweli ilikuwa
vigumu kwa kiungo huyo wa zamani wa Chelsea kuweza kufanya kitendo hicho kwani
kwa msaada ya video, alionekana akiongea mfululizo wakati akikabiliana na
mwamuzi
Meireles, kwa
nguvu zote alipinga adhabu hiyo na alikuwa akitaka adhabu hiyo kama si kuondoshwa
basi ipunguzwe.
Alikaririwa
akisema,
"hukumu imekwisha tolewa wakinishutumu mimi kufanya kitu ambacho
sikufanya. Sikuwahi kumtemea mwamuzi mate.
Aidha klabu
ya Galatasaray, imeshutumu maamuzi ya kupunguzwa kwa adhabu hiyo kulikofanywa
na mahakama ya usuluhishi, taarifa ya klabu hiyo kupitia mtandao wa klabu imesomeka
kwa kichwa cha habari “ ni aibu kwa soka la Uturuki ".
Taarifa hiyo
imeendelea kusema
"kwa
kumpunguzia adhabu Raul Meireles michezo minne ni kwamba kamati imepuuza
ushahidi wa wazi'
"punguzo
la adhabu ambayo imetokana na taarifa ya kweli ya mwamuzi, kushindwa kabisa, si
tu kwa jamii nzima ya soka , lakini pia kwa fani nzima ya uamuzi. "
No comments:
Post a Comment