KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, December 14, 2012

Shinji Kagawa arejea mazoezini na Nimanja Vidic kunguruma dhidi ya Sunderland kesho.SIKU ZA LAMPARD CHELSEA ZINAHESABIKA na Juan Jesus anasema Inter lazima achukue Scudetto.

Frank Lampard ameweka wazi kuwa siku za utumishi wake katika klabu ya Chelsea sasa zinahesabika wakati huu ambapo maekuwa ni sehemu ya wachezaji wa kocha wa muda Rafa Benitez.
 
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 ambaye amekuwa mtumishi katika klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 10, alikuwa na matumaini ya kumaliza kabisa uchezaji wake wa soka katika klabu hiyo ambayo amefanikiwa kutwaa mataji 3 ya ligi kuu ‘Premier League’, mataji manne ya kombe la FA na msimu uliopita akifanikiwa kushinda taji kubwa la vilabu barani ulaya ‘UEFA Champions League’.
Amenukuliwa na Telegraph akisema,
"nadhani nina miaka miwili au mitatu ambayo nitaendelea kuwepo katika kiwangu cha juu, Pengine mambo hayawezi kudumu milele”

Akiwa amefunga mabao karibu 200 akiwa na Chelsea Lampard anajivunia kuwepo Stamford Bridge katika kipindi chote akiwa hapo na ana amini kuna mengi ambayo ameyafanya ikiwa hata kutwaa taji la vilabu ulaya.

Juan Jesus anasema Inter lazima achukue Scudetto.
Mlinzi wa Inter Milan Juan Jesus amesema kuwa kikosi kima cha timu yao kinaamini kuwa wanauwezo wa kutwaa taji la ligi kuu ya nchini Italia ‘Scudetto’, namkuweka wazi kuwa kila mmoja amejidhatiti kuhakikisha Juventus inaondoka katika uongozi wa ligi Serie A.
Wakiwa nyuma kwa alama nne, bado mlinzi huyo wa kimataifa wa Brazil anaamini kuwa wachezaji wenzake watafanya kila linalo wezekana kutwaa taji hilo ambalo wanalisaka tangu mwaka 2010.
Akiongea na Sport Mediaset amekaririwa akisema,
"siku zote tunaamini kuwa tunaweza kushinda Scudetto, na ninataka kufanya kila kitu kinachowezekana kulinyakua taji hilo"

 "Inter ni klabu kubwa tutafanya kila linalo wezekana kushinda"

Pia mlinzi huyo amezungumzia jinsi alivyo fanikiwa kuyazoea maisha ya nchini Italia na sasa anaeleza wazi kutamani kuendelea kuishi San Siro kwa muda mrefu.
"ninafurahia kwasababu kulikuwa hakuna mtu aliyekuwa ananijua hapa Italia lakini sasa mambo yamebadilika. Ninatamani kuwa na miaka mingine zaidi mitano au sita kuonyesha uwezo wangu. Nataka kuwa sehemu ya Inter kwa muda mrefu.

 Shinji Kagawa arejea mazoezini .Nimanja Vidic kunguruma dhidi ya Sunderland kesho.
Meneja wa mashetani wekundu Manchester United Sir Alex Ferguson amethibitisha kuwa kiungo wake has confirmed that midfielder Shinji Kagawa atarejea katika mazoezi yake kama kawaida wiki ijayo kwa kuwa hivi sasa anaendelea vizuri.
Kiungo huyo aliyesajiliwa msimu wa uhamisho wa kiangazi akitokea Borussia Dortmund amekuwa nje ya uwanja tangu Oktoba wakati United ilipocheza dhidi ya Braga mchezo wa vilabu bingwa Ulaya ambapo Kagawa alipatwa na maumivu ya mguu.
Pia kuna taarifa njema kwa mashabiki wa United ambapo Nemanja Vidic nikiwa kuimarisha afya yake na anatarajiwa kuwepo dimbani jumamosi katika mchezo dhidi ya Sunderland utakaopigwa Old Trafford.
Mzee Furgauson amenukuliwa akisema
"Nemanja anarejea kikosini kesho , lakini Jonny Evans ni wazi kuwa atakuwa nje baada ya maumivu ya wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment