KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, December 15, 2012

SIMBA KUMSAJILI MRITHI WA SUNZU KUTOKA CAMEROON, AGIZO LA KOCHA MPYA BABU PATRICK LIEWIG

Kocha mpya wa klabu Simba Patrick Liewig ameutaka uongozi wa klabu ya Simba kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Camerron ambaye jina na wasifu wa mshambuliaji huyo umewasilishwa katika uongozi wa klabu hiyo.

Akiongea na Rockersports afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kocha Liewig katika kuhakikisha Simba inafanya vizuri katika michuano ya vilabu barani Afrika amewataka kumsajili mshambuliaji huyo ambaye anaamini ataisaidia Simba.

Hata hivyo Kamwaga hakuwa tayari kumtaja mshambuliaji huyo na klabu anayotoka lakini ameihakikishia Rockersports kuwa uongozi wa Simba kupitia kamati yake ya usajili chini ya Zakaria Hans Pope uko katika hatua nzuri kumleta mshambuliaji huyo nchi ambaye pia anatarajiwa kuziba pengo la mshambuliaji raia wa Zambia aliyeondoka Felix Sunzu.

“Yah ni kweli Patrick Liewig aliwataka washambuliaji wawili majina tunayo, na sasa uongozi wa Simba kupitia kamati ya usajili chini ya Hans Pope wanaendelea na mchakato, tatizo hapa ni kwamba dirisha dogo linafungwa kesho(leo) hivyo bado tunaangalia sheria za dirisha dogo zikoje? Lakini kamati yetu ya usajili imeshawasiliana na mmoja wa washambuliaji hao”
“Tunaamini  watakuwa ni wachezaji wazuri kwa mujibu wa taarifa ambazo kocha ametupatia, na namna ambavyo kamati inavyo shughulikia”
Kocha mpya Patrick Liewig anatarajiwa kuwasili nchini baada ya sikukuu ya Chrismass, ambapo atasaini mkataba rasmi, tayari kuanza kuifundisha klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi.