Mabingwa wa
soka Tanzania Bara wekundu wa Msimbazi Simba hii leo wamekubali kichapo cha mabao 3-0 toka
kwa mabingwa wenzao wa nchini Kenya Tusker katika mchezo uliofanyika katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba ambayo
iliwatumia zaidi wachezaji wake wa kikosi cha pili hususani katika kipindi cha
kwanza ikiwa chini ya makocha makocha Moses Basena na Jamhuri Kihwelu ilikubali
mabao mawili katika kipindi hicho yaliyofungwa na Jesse Were kunako dakika za 37 na
45.
Tusker
iliandika bao la tatu kunako dakika ya 54 lilofungwa na Frederick Onyango.
Simba ambayo
inajiandaa na safari ya kuelekea Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la
Mapinduzi ilikuwa ikicheza mchezo huo bila ya mpangilio wa kueleweka ikiwatumia
akina Haruna Shamte, Haruna Athumani, Paul Ngalema, Mussa Mudde, Abdallah
Seseme, Abdallah Juma, Ramadhani Chombo, Kiggi Makassy na Miraj Adam.
Wengine ni Hassan
Isihaka, Emily Ngeta, Jonas Mkude, Salim Kinje, Haruna Moshi, Ramadhani
Singano, Nassor Masoud ‘Chollo’ na Edward Christopher.
Simba hii
leo iliwakosa wachezaji wake muhimu kadhaa kama Juma Kaseja, Shomari Kapombe na
Emmanue Okwi.
Tusker FC
iliwatumia Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright, Mark Odhiambo,
Joseph Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Manono, Frederick Onyango, Ismail Dunga,
Jesse Were, Robert Omonuk,
Baada ya
mechi hiyo Kocha wa Tusker Robert Matano alisema kwamba hatua ya timu yake
kupata ushindi katika mechi mbili ngumu, imempa faraja ya kunyakua ubingwa wa
Kombe la Mapinduzi inayotarajia kuanza January 01 mwaka 2013 visiwani Zanzibar.
Naye Kocha
wa Simba Julio alisema kwamba hatua ya Simba kupotea mechi hiyo imempa nafasi
ya kujua makosa ya timu na atayarekebisha kabla ya kombe la Mapinduzi kuanza.
No comments:
Post a Comment