KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, December 29, 2012

UKURASA WA HABARI ZA KIMATAIFA: Maradona: Mourinho ni miongoni mwa makocha bora duniani, Anzhi yapuuza tetesi za kutenga euro milioni 250 kumsajili Messi, Rosell: Tito Vilanova atarejea ndani ya siku 15 mpaka na Guardiola kufundisha mwaka 2013..



Diego Maradona anaamini kuwa kocha wa Real Madrid ni miongoni mwa makocha bora duniani.


Mreno huyo aliiongoza Blancos mpaka kutwaa taji la ligi kuu nchini Hispania La Liga msimu uliopita na pia akiwa na rekodi ya kutwaa mataji katika nchi zenye ligi ngumu kama vile Ureno, England na Italia pamoja na kutwaa mataji mawili ya vilabu bingwa Ulaya.


Maradona, ambaye katika fani ya ufundishaji hakung’ara sana kama ilivyokuwa katika kipindi cha uchezaji wake, anaamini kuwa bosi huyo wa zamani wa Inter katika kipindi chote amefanikiwa kuwa juu.


Akinukuliwa nchini Dubai hapo jana Maradona amesema,

"matokeo aliyoyapata Mourinho yanaongeza nguvu ya sauti ya uwezo wake”

Ameendelea kwa kusema nimekuwa nikimuona akifundisha katika kiwango cha juu, amekuwa makini na kila mchezaji katika kikosi chake kuanzia mwanzo mpaka mwisho.


"nilikuwa ni mchezaji niliyekuwa nataka kujulikana, lakini ni jambo jema kuona kocha hakujali peke yako lakini timu nzima kwasababu wao ndio wanao kusaidia uwanjani"

Maradona kwasasa hana timu ya kufundisha baada ya kuondoshwa katika klabu ya Al Wasl mapema mwaka huu wa 2012.


Nafasi kubwa aliyopata katika ufundishaji wake ni timu yake ya taifa ya Argentina mwaka 2010 katika fainali ya kombe la dunia, ambapo timu hiyo ya taifa kutoka Amerika ya kusini ilitolewa na Ujerumani katika robo fainali.



Anzhi yapuuza tetesi za kutenga euro milioni 250 kumsajili Messi
 Anzhi Makhachkala imekanusha taarifa zilizowahusisha kuwa wametenga euro milioni 250 kwa ajili ya kumsajili nyota wa Barcelona Lionel Messi.


Taarifa zilizo ripotiwa na jarida la Mundo Deportivo ziliarifu kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina amekataa ofa ya euro milioni 30 kutoka katika klabu hiyo ya Russia.



Hata hivyo mshauri wao wa mambo ya masoko, German Tkachenko ameponda taarifa hiyo na kusema ilikuwa ni uongo mtupu na kusisitiza kwamba klabu yake haifanyi shughuli za uhamisho kwa namna hiyo.

Akiongea na gazeti la Russia la Sports-Express amesema

"hakuna hata chembe ya ukweli katika hilo"

Gazeti hilo la nchini Russia pia limearifu kuwa Messi si tu amekataa ofa hiyo, lakini pia kama mpango huyo ungefanikiwa basi mkataba wake ungemuweka katika klabu hiyo mpaka 2018.


Mshambuliaji mwenzake wa zamani wa Camp Nou Samuel Eto’o, ambaye alicheza pamoja na Messi  Barca, aliondoka Russia na kuelekea katika klabu hiyo kwa mshahara mnono akiwa ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa duniani na alihama kwa uhamisho wa euro milioni 20 kwa mwaka.



 Rosell: Tito Vilanova atarejea ndani ya siku 15 mpaka.
 Rais wa Barcelona Sandro Rosell metanabaisha kuwa kocha wake Tito Vilanova atarejea katika kazi yake ya umeneja ndani ya kipindi cha wiki tatu.

Kocha huyo alikuwa nje ya kazi tangu katikati ya mwezi huu, baada ya kutakiwa kufanyiwa upaasuaji baada ya kugundulika na kansa kwa mara ya pili.

Rosell ana matumaini kuwa kocha huyo msaidizi wa zamani chini ya Pep Guardiola ataweza kufanya matibabu yake madogomadogo wakati akiendelea na ukocha wake, lakini amesisitiza kuwa kupona kwa Vilanova ndio jambo la kipaumbele kuliko mpira.


Rais huyo wa Barca alikuwa akiongea na waandishi wa habari mjini Dubai ambapo alinukuliwa akisema

 “atakuwa akifanya vyote matibabu na kufundisha licha ya kwamba kipaumbele ni afya yake."

Rosell alikwepa kuelezea kama Xavi na Carles Puyol watapewa mikataba mipya Camp Nou, lakini amesisitiza kuwa angependa kuona Barca ikiendelea kuwa nao kikosini.



Guardiola kufundisha mwaka 2013.
 Pep Guardiola atarejea kufundisha soka mwakani 2013 baada ya muda mrefu nje ya soka kwa mujibu wa Rais wa zamani wa Barcelona Joan Laporta.

Guardiola aliondoka kuifundisha Barcelona baada ya kumalizika msimu uliopita akitaka kupumzika kwa muda baada ya misimu minne ya kuifundisha kwa mafanikio vijana wa Catalunya.


Kocha huyo raia wa Hispania alikuwa akihusishwa na kujiunga na moja ya vilabu vukubwa barani Ulaya tangu wakati ho alipoa achana na Barcelona, ikiwa ni pamoja na Paris Saint-Germain, ingawa Laporta anaamini kuwa klabu hiyo ya nchini Ufaransa haimfai Guardiola.


Akikaririwa amesema

"nadhani Pep atarejea kufundisha mwakani. Ana mvuto mkubwa wa kufundisha, ana mawazo safi na ana akili"
 Najisikia mwenye heshima kuwa karibu na Pep, kwangu mimi ndiye kocha bora dunia.

No comments:

Post a Comment