Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) imezipongeza timu za Ashanti United ya Dar es Salaam, Mbeya City
ya Mbeya na Rhino Rangers ya Tabora kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu
ujao (2013/20114).
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wallace Karia amezitaka
timu hizo kufanya maandalizi ya kutosha ili ziweze kushindana katika VPL
ikiwemo kutimiza masharti ya kuwa klabu za Ligi Kuu.
Moja ya masharti ya klabu zenye hadhi ya Ligi Kuu ni
kuwa na timu ya pili (U20) ambayo itakuwa na inacheza mechi za utangulizi
kwenye uwanja wa nyumbani kila timu ya wakubwa inapocheza.
Mbali ya kuthibitisha timu hizo tatu kupanda daraja,
pia Kamati ya Ligi imethibitisha rasmi timu tatu zilizoshuka daraja kurudi Ligi
ya Mkoa katika mkoa husika. Timu zilizoshuka kutoka Daraja la Kwanza (FDL) ni
Small Kids ya Rukwa kutoka kundi A.
Kundi B timu iliyoshuka ni Moro United ya Dar es
Salaam wakati Morani FC ya Manyara yenyewe imeporomoka kutoka kundi C.
No comments:
Post a Comment