![]() |
Tony Bellew anadhani alistahili ushindi katika mchezo wake dhidi ya Isaac Chilemba. |
Mchezo wa marudiano wa masumbwi baina ya Tony Bellew dhidi ya Isaac
Chilemba utachezwa Mei 25 katika ukumbi wa O2 Arena likiwa ni pambano la utangulizi la Carl
Froch dhidi ya Mikkel Kessler.
Pambano hilo lenye mvuto mkubwa la jijini Liverpool la uzito mwepesi wa juu lilimalizika kwa sare mwezi uliopita.
Taarifa zinasema kuwa mshindi wa pambano hilo atakuwa akimsubiri mshindi wa pambano la kusaka mshindi la WBC
baina ya Chad Dawson dhidi ya Adonis Stevenson litakalochezwa Juni 8.
Mtayarishaji Eddie Hearn ameweka wazi hilo kuwa mabondia wote wako tayari kwa mchezo wa marudiano haraka iwezekenavyo.
Amenukuliwa akisema.
'Hakukuwa na mshindi na sisi tunataka mshindi '
'Watu wengi walidhani Tony alishinda na wengine walidhani Chilemba alishinda katika pambano lililopita. Ni pambano ambalo inabidi kuyasahau yaliyopita'

Wakati huohuo mpinzani wa George Groves ambaye atacheza pambano lingine la utangulizi usiku huo atatangazwa wiki hii.
No comments:
Post a Comment