Timu ya taifa ya Nigeria "Super eagles" imeshindwa kufanya safari ya kuelekea nchini Brazil kufuatia wachezaji wa timu hiyo kutokulipwa bonasi zao.
Super Eagles inatarajia kuanza mchezo wake wa kwanza wa michuano ya kombe la shirikisho la mabara jumatatu ambapo wamesalia nchini Namibia ambako walikuwa akicheza mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia hatua ya makundi dhidi ya Namibia.
Wachezaji wa hawana furaha baada ya kupewa kila mmoja dola $2,500 (sawa na pauni £1,590) za bonasi waliyo ahidiwa baada ya kwenda sare ya ugenini ya bao 1-1mjini Windhoek, na kusisitiza kuwa wanataka iwe mara mbili.
Timu hiyo imegoma kusafiri huku mgomo ukiendelea.
Sakata hilo limeibua maswali endapo mabingwa hao wa Afrika watashiriki michuano hiyo ambayo itaanza june 15 mpaka 30.
Rais wa shirikisho la soka la Nigeria(NFF) Aminu
Maigari alikutana na timu hiyo usiku wa jana mjini Windhoek kuwaelezea kuwa shirikisho lake halina maamuzi mengine zaidi ya kupunguza matumizi.
Wiki iliyopita vyombo vya habari viliarifu juu ya mzozo na dhamira ya kugoma kutokana na tatizo la bonasi baada ya Super Eagles kuichapa Kenya jijini Nairobi kwa bao 1-0 katika mchezo mwingine wa kusaka nafasi ya kufuzu kombe la dunia.
Wchezaji walitaka kulipwa dola $10,000 (sawa na £6,370) kila mmoja kwa ushindi huo wa Nairobi lakini maafisa mbalimbali walikanusha madaia hayo.
Nigeria walitarajia kuondoka Windhoek kuelekea Johannesburg Afrika kusini kabla ya kuelekea Sao Paulo nchini Brazil hii leo ambapo mchezo wa kwanza wa ufunguzi utakuwa ni dhidi ya Tahiti.
No comments:
Post a Comment