Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amekanusha taarifa kuwa anajipanga kusaini mkataba mpya na klabu yake hiyo.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa akihusishwa na kutaka kuelekea klabu ya Monaco ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 85.
Mkataba wa sasa wa mreno huyo utamalizika 2015 lakini Rais wa Real Madrid Florentino Perez amekuwa akipendezwa na kumuongezea makataba wakati huu wa majira ya kiangazi ili astaafu soka akiwa ndani ya klabu hiyo.
Safari ya Ronaldo katika soka
- Sporting Lisbon: 2002-03
- Manchester United: 2003-2009: Premier League 2007, 2008, 2009; FA Cup 2004; League Cup 2006, 2009; Champions League 2008
- Real Madrid: 2009-present: La Liga 2012; Copa del Rey 2011; Supercopa de Espana 2012
Katika hatua nyingine Ronaldo ambaye alijiunga na Madrid june 2009 kwa ada ya uhamisho ya kihistoria ya pauni milioni 80 akitokea Manchester United, ameandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa tweeter kuwa"
"Habari zote juu ya kusaini tena na Real Madrid ni za uongo."
Ronaldo ameitumikia Bernabeu kwa misimu minne na kufunga jumla ya magoli 201 katika jumla ya michezo 199 ya mashindano yote na kuisaidia kutwaa taji la ligi ya Hispania La Liga
msimu wa 2011-12.
No comments:
Post a Comment