Kiungo wa timu ya taifa ya Misri na klabu ya Al Ahly Mohamed Barakat ametangaza kuwa atastaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36 ameitumikia Al Ahly jumla ya michezo 173 na kuifungia magoli 34 tangu ajiunge nayo akitokea Ahly Jeddah ya Saudi mwaka 2004.
Ameichezea timu ya taifa ya Misri maarufu kama Mapharao jumla ya michezo 70 na kufunga jumla ya magoli nane.
Amenukuliwa kupitia mtandao wa klabu hiyo akisema:
"Nimeamua leo kumaliza soka lakini nitaendelea kuwa na Al Ahly mpaka mwisho wa msimu huu".
"Nina matumini nimeitendea haki Al Ahly."
Kocha wa Ahly Mohammed Youssef ametanabaisha kuwa ana imani Barakat ataongeza msimu mwingine mmoja.
"Ni mchezaji mkubwa na hivyo ni vigumu kumsahau"
Akiongea na mtandao wa klabu hiyo Youssef amsema anaheshimu maamuzi ya mchezaji huyo na anamtakia kila la kheri hapo baadaye.
Barakat aliaanza kucheza soka katika klabu ya Al-Sekka Al-Hadid mwaka 1996
na pia ameichezea vilabu vya Ismaily, Arabi na Ahly Jeddah kabla ya kujiunga na Ahly, ambako amekuwepo kwa miaka tisa.
Akiwa na Ahly, ameshinda taji la ligi ya Misri mara saba na ubingwa na Afrika mara tatu ambapo mwaka 2005 alikuwa mfungaji bora wa mashindano hayo akifunga jumla ya magoli saba.
Barakat amefikia mafanikio makubwa katika hatua ya soka la kimataifa kwa kushinda taji la mataifa ya Afrika akiwa na timu ya taifa ya Misri mwaka 2006.
Heshima binafsi aliyopata ni mwaka 2002 na 2009 alitangazwa kuwa mchezaji bora wa Misri na mwaka 2005 aliibuka kuwa mchezaji bora wa tuzo ya BBC barani Afrika.
No comments:
Post a Comment