Braza la vyama vya soka kwa nchi za Afrika mashariki na kati
(Cecafa) limetangaza timu tatu ambazo zitachukua nafasi ya timu ambazo zimejitoa katika mashindano yajayo ya kombe la Kagame yatakayo fanyika nchini Sudan.
Bingwa wa Kenya Tusker FC na timu mbili za Tanzania Simba na mabingwa watetezi wa taji hilo Yanga zilitangaza kujitoa katika mashindano hayo kutoka na kile kilicho elezwa kuwa hali ya usalama hairidhishi katika miji mwenyeji ya Durfur na South Kordofan.
Katibu wa Cecafa Nicholas Musonye amezitaja timu za Uganda Revenue Authority URA ambao walikuwa wawakilishi wa Uganda katika michuano ya vilabu bingwa Afrika na ambao walimaliza katika nafasi ya pili katika ligi ya Uganda pamoja na Rayon Sport ya Rwanda na Elect Sport ya Chad zitachukua nafasi ya zile zilizo jitoa.
Musonye ameelezea imani yake kuwa June 18 mpaka July 2 michuano hiyo itakuwa salama.
Amenukuliwa akisema kuwa
"Wamefanya safari kuelekea Darfur na South Kordofan na kwamba usalama ni mzuri. Hakuna haja ya mtu kukaa Nairobi au
Dar es Salaam na kudhani usalama ni mbaya.
"Haya ni mashindano makubwa na tulijarabu kuzishawishi serikali za Kenya na Tanzanian kuwa usalama upo lakini wamekataa kutuamini"
Musonye ameongeza kwamba mabadiliko yatafanyika katika makundi baada ya wajumbe wa Cecafa na wenyeji shirikisho la soka la watakapo kutana mjini Khartoum mwishini mwa juma.
Michuano hiyo inayodhaminiwa kwa sehemu na Rais wa Rwanda Rwanda Paul Kagame,sasa itakuwa na timu zifuatazo:
Al Ahly Shandi (Sudan), Al Nasir (South Sudan),
Al-Hilal Kadugli (Sudan), Express FC (Uganda), URA FC (Uganda), Ports FC
(Djibouti), Vital'O (Burundi), Merriekh El Fasher (Sudan), APR
(Rwanda), Elman (Somalia), Rayon Sport (Rwanda) and Elect Sport (Chad).
No comments:
Post a Comment