KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, June 14, 2013

IVORY COAST WANA STRESS YA KUGOMBANA WENYEWE KWA WENYEWE. WAMEMFUKUZA RAZAK KWA KUPIGANA KAMBINI.

'I thought we'd finished this': Toure looks on in disbelief as Razak and Gosso grapple with eachother.
 
Kiungo chipukizi wa Ivory Coast na Manchester City Abdul Razak ametimuliwa kikosini na kurejeshwa nchini Ivory Coast kufuatia kupigana na mchezaji mwenzake wa Ivory kabla ya kufanya safari ya kuja Tanzania kwa ajili ya mchezo wa hatua ya makundi kusaka nafasi ya kucheza fainali ya kombe  dunia.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 aliaadhibiwa kwa kurejeshwa nyumbani kufuatia kupigana na Jean-Jacques Gosso, ambaye anachezea klabu soka nchini Uturuki katika klabu ya Mersin Idmanyurdu, wakati wakiwa mazoezini kabla ya mchezo wao dhidi ya Tanzania utakao fanyika jumapili.
Gosso pia amepewa onyo kufuatia ugomvi huo ambao ulishuhudiwa na kiungo nyota wa Man City Yaya Toure,

Kiungo huyo mwenye uwezo wa kumiliki vema mpira na ambaye alifunga moja katika ushindi wa Ivory Coast wa mabao 3-0 dhidi ya Gambia wiki iliyopita , hakuonyesha kushangazwa na ghasia hizo za wakati wa mazoezi kwani alikwisha shuhudia ugomvi mwingine katika klabu yake ya Manchester City ikiwa ni pamoja na mizozo mingine kama ya akina Mario Balotelli, Jerome Boateng, Micah Richards na meneja wa zamani wake Roberto Mancini ndani ya viunga vya Carrington.

UGOMVI ILIYOSHUHUDIWA NA YAYA TOURE NI HII IFUATAYO

kulikuwepo na ugomvi kama 

Baloteli v Boateng 2010

Tevez v Mancini 2010

K Toure v Adebayo 2011

Balotelli v Komapany 2011

Balotelli v Mancini 2012

Wakati wa tukio hilo la hivi karibuni la kambini timu ya taifa ya Ivory Coast, kiungo huyo alikuwa kwa nyuma akingalia kwa huzuni ugomvi huo ukitokea mbele ya macho yake katika uwanja wa Felix Houphouet Boigny mjini Abidjan jumatano.

Razak aliondoka kikosi cha na kujiunga City mwaka 2008 bado hajajitengenezea nafasi ya kucheza Etihad Stadium.

No comments:

Post a Comment