Manchester City wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo mchezeshaji wa Malaga Isco ukiwa ni usajili wao wa tatu katika msimu huu wa usajili wa kiangazi.
City wanaamni kuwa mambo ya msingi ya makubaliano ikiwa ni pamoja na maslahi binafsi ya mchezaji huyo yatakubaliwa na kiungo huyo anayechipukia wa kikosi cha timu ya taifa cha Hispania cha umri chini ya miaka 21, ambaye anatakuwa akimfuata Manuel Pellegrini katika viunga vya Etihad wiki zijazo.
Kocha raia wa Chile Pellegrini aliihama Malaga mwishoni mwa msimu uliopita na mabingwa hao wa ligi ya England msimu wa 2012
wanatarajia kumtangaza Pellegrini mwishini mwa juma.
Isco mchezaji wa Hispania Under 21 (kushoto) anakaribia kujiunga na Manchester City.
Isco mwenye miaka 21, alingara katika ligi ya hispania La Liga na ligi vilabu bingwa Ulaya akiwa na Malaga lakini sasa amedokeza juu ya azma yake ya kuondoka Hispania.
City pia wanamtaka mshambuliaji wa Napoli Edinson Cavani.
No comments:
Post a Comment