Julio Cesar katika rada ya Arsenal baada ya kumaliza mpango wake na Queens Park Rangers' iliyoshikia daraja. |
Arsenal inajipanga kukamilisha usajili wa mlinda mlango Cesar lakini ianonekana bado wanachanganyikiwa na jinsi ya kunasa saini za Fellaini na Williams
Arsenal inajipanga kukamilisha uusajili wa mlinda mlango wa Queens Park Rangers Julio Cesar baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la mabara.
Arsene Wenger anataka mlinda mlango mzoefu kuongeza ushindani kwa walinda milango wake makinda Lukasz Fabianski na Wojciech Szczesny.
Mazungumzo baina ya mwakilishi wa Cesar na mkuu wa washika mitutu hao yameshafanyika lakini kwasasa kinachoendelea ni kusubiri mlinda mlango huyo amalize michuano ya kimataifa.
The Gunners are now actively trying to complete the swoop after Italian side Roma joined the race to land Cesar.
Mlinda mlango huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye yuko huru kuondoka katika viunga vya Loftus Road kufuatia ushuka daraja kwa QPR anatazamaiwa kusalia katika jiji la London tangu aliwasili hapo akitokea Inter Milan msimu uliopita.
Wakati washika mitutu wakiwa pia na matumaini ya kukamilisha usajili wa Gonzalo Higuain wiki ijayo, baada ya meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti kuweka wazi kuwa mshambuliaji huyo anaweza kuondoka Arsenal ina imani kuwa mpango huo unaweza kukamilika baada ya fainali ya kombe la mabara hapo kesho.
Wenger
anafikiria pia kumnasa nyota wa Stoke City Asmir Begovic na Pepe
Reina huku wakiwa na pauni milioni £70 kwa ajili ya kufanya usajili.
No comments:
Post a Comment