Emmanuel Okwi |
Klabu ya Simba na Etoile du Sahel ya Tunisia zimefikia makubaliano ya kumaliza tatizo la malipo ya fedha za malipo ya mauzo ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emannuel Okwi ambaye klabu ya Simba ilimuuza kwa klabu hiyo.
Akiongea na mtandao wa Rockersports akiwa Tunis Tunisia alikokwenda kufuatia fedha hizo, mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Zackaria Hans Poppe amesema kuwa kimsingi wamefikia muafaka wa suala hilo ambapo Simba inaidai Du Sahel dola milioni 350 ambazo klabu hiyo kubwa nchini humo na barani Afrika kwa ujumla imeafiki kulipa fedha hiyo bila kutaja ni lini hasa fedha hizo zitatolewa.
Amesema anatarajiwa kulipeleka suala hilo kwa uongozi wa Simba uliomtuma kufuatialia fedha hizo na baadaye litakwenda kamati ya utendaji ambayo italijadili na hatimaye kuwafikia waandishi wa habari.
Kikao baina ya Hans Poppe na uongozi wa Etoile du Sahel kilimalizika jana usiku ikiwa ni muda mfupi kabla ya kuongea na mtandao huu wa Rockersports ambapo Hans Poppe alikanusha taarifa kuwa malipo ya Okwi yatafanyika mwezi Septemba kama ilivyo arifiwa katika baadhi ya vyombo vya habari.
Okwi mzaliwa wa jiji la Kampala nchini Uganda mwenye umri wa miaka 20, alijiunga na Simba msimu wa mwaka 2010/2011 akitokea Sports club Villa ya Uganda ambapo aliitumikia klabu hiyo mpaka mwezi januari mwaka 2013.
Akiwa na klabu ya Simba aliichezea klabu hiyo jumla ya michezo 72 ambapo aliifungia jumla ya mabao 26 katika michezo yote ya ligi kirafikia na mashindano ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment