Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari amesema
kikosi chake hakina majeruhi hata mmoja baada ya mchezo wa nusu fainali dhidi
ya Uruguay na huenda akatangaza kikosi kilekile kilichocheza katika mchezo wa
nusu fainali kuanza katika fainali ya hapo kesho.
Hulk mpaka sasa ameshindwa kuweka
mpira wavuni katika jumla ya michezo tisa ya kimataifa hii ikiwa ina maana kuwa
nafasi yake kuaza kikosini ni finyu ikilinganishwa na wakali kama Bernard na
Lucas Moura.
Roberto Soldado na Cesc Fabregas katika
kikosi cha Hispania walikosekana katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Italia
kutokana na maumivu madogo ya msuli hivyo inanyoonekana ni kwamba wachezaji hao
wawili wanaweza kuanza hapo kesho.
MATCH
PREVIEW
Hispania wametajwa kama ni timu
ambayo imetinga hatua hiyo kwa bahati sana lakini wengine wanasema ni fainali
iliyokuwa katika ndoto za wapenzi wengi wa soka ni itakuwa na mvuto wa aina
yake pale Maracana .
Wakati Italia ikitajwa kuwa ndiye
aliye onyesha upinzani wa kweli kwa Selecao ukweli ni kwamba Azzurri walisha kutana mara mbili na Brazil mwaka
huu lakini bado mawaidha ya wengi ni kwamba hii itakuwa ni "dream
final" baina ya Brazil na Hispania.
Brazil na Hispania kwa ajabu ya
wengi kwamba wamekutana mara moja tu katika kipindi miaka 23 iliyopita na hiyo
ilikuwa ni mwaka 1999 katikia mchezo wa kirafiki ambao walikwenda sare ya bila
kufungana.
Tangu wakati huo Hispania imekuwa
ikifanya vizuri na kuwachapa yeyeto anayetokeza.
Brazil ndiyo taifa ambalo ni kubwa
kisoka anayedaiwa kulinganishwa naye kama mbabe na mchezo huu unatazamwa kama
ndiyo kipimo tosha kwa mataifa hayo.
Ushindi wa Hispania dhidi ya Brazil
ambao hawajapoteza katika uwanja wa nyumbani tangu mwaka 1975, utadhihirisha
ukubwa wao katika soka la dunia ya leo.
Vuta kumbukumbu miaka 63 iliyopita
ambapo Hispania ilibamizwa kwa kichapo cha karaha cha mabao 6-1 katika dimba la
Maracana matokeo ambao yaliondoa matumaini yao ya kutwaa kombe la dunia mwaka 1950
na kusalia katika kumbukumbu kuwa ni kichapo kikubwa mno kuwahi kuwakumba
katika michuano mikubwa.
Kwa kuongezea hili la faida ya
kucheza katika uwanja wa nyumbani Brazil itafaidika na hilo.
Kocha wa Hispania Vicente del Bosque
anasema mchezo mgumu dhidi ya Italia wa nusu fainali umeivuruga kambi yake
lakini wanasonga mbele.
Brazil's
record against Spain
- 1934 World Cup first round: Lost 3-1
- 1950 World Cup final round: Won 6-1
- 1962 World Cup group stage: Won 2-1
- 1978 World Cup: Drew 0-0
- Friendly, 1981: Won 1-0
- 1986 World Cup: Won 1-0
- Friendly, 1990: Lost 3-0
- Friendly, 1999: Drew 0-0
No comments:
Post a Comment