Andre Villas-Boas kwa mara nyingine amedai kuwa Gareth Bale haendi popote kiangazi hii licha ya gazeti ya Hispania la Marca kudai kuwa raia huyo wa Wells ambaye wamemwita mchawi wa Wells anaelekea kujiunga na Real Madrid na kwamba zoezi hilo limekamilika.
Gazeti hilo la nchini Hispania limedai kuwa Real wanakaribia kabisa kuingia mkataba wa mchezaji huyo mkataba wa miaka sita wenye thamani ya pauni milioni £8.5 kwa mwaka.
Marca pia limedai kuwa Bale amemwambia kiongozi wa juu wa Spurs kuwa anataka kuelekea Bernabeu.
Villas-Boas, ameongea hayo wakati wakiwa katika harakati za kuelekea katika Barclays Asia Trophy, ambapo kwa mara nyingine tena ametupilia mbali juu ya uwezekano wa Bale kuondoka lakini amethibtisha kuwa klabu yake iko katika mawindo ya kunasa saini ya mshambuliaji wa Valencia Roberto
Soldado.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Hong Kong
asubuhi hii, Villas-Boas ametanabaisha kuwa Bale hatakuwepo katika mchezo wa kesho dhidi ya Sunderland baada ya kukumbwa na majeraha akiwa mazoezini.
Bosi wa Spurs amenukuliwa akisema
‘Nataka kurudia tena kauli yangu kuwa yale niliyo yasema msimu uliopita na yale niliyo waambia wakati wa kuanza maadalizi ya msimu ndiyo hivyo hivyo siwezi kueleza zaidi ya hapo.
No comments:
Post a Comment