KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, July 8, 2013

Liverpoo yakataa ofa ya Arsenal ya pauni milioni 30 kumnasa Suarez, Swansea yakaribia kumsajili Wilfried Bony, Eric Abidal ajiunga na Monaco baada ya kuachwa na Barcelona,Arouna Kone asajiliwa na Everton akitokea Wigan Athletic na Mshambuliaji wa Bayern Munich Mario Gomez kujiunga na Fiorentina.



 Liverpool imepiga chini ombi la klabu ya Arsenal la kumtaka mshambuliaji wake Luis Suarez kwa ada ya pauni milioni.
Suarez amekuwa katikati ya tetesi za kuhama klabu hiyo tangu aliposema kuwa ana mpango wa kuhama mwezi wa Mei alipotumia maneno kuwa it would be a "good moment for a change", na kutumia maneno maengine kuwa "difficult to say no" kujiunga na Real Madrid.
Real Madrid ilikuwa ikitazamiwa kuelekeza ushawishi wao wa kumsawishi mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26-raia wa Uruguay.
Liverpool imekataa kuzungumza lolote juu ya taarifa ya Arsenal huku wakisisitiza kuwa Suarez is not for sale.
Chelsea pia walikuwa wakihusishwa na kumtaka Suarez na ilikuwa ikionekana kuwa Arsenal walikuwa vinara wa hilo ambapo meneja Arsene Wenger alikuwa akiendelea kumalizia mchakato kwanza wa Gonzalo Higuain wa Real Madrid.
Real wanatazamiwa kuathirika na kauli hiyo ya Liverpool ya kwamba Suarez hauzwi vinginevyo labda ni kwa ada ya pauni milioni £50 ambayo ilimng’oa Fernando Torres alipojiunga na Chelsea mwezi January 2011.

Swansea yakaribia kumsajili Wilfried Bony
 Swansea City wanatarajiwa kumsajili mshambuliaji mduchi Wilfried Bony kutoka Vitesse Arnhem zoezi ambalo huenda likamalizwa hii leo.
Mpango huo huenda ukagharimu kiasi cha pauni milioni £13 kutegemeana na mahitaji mengine binasfi yaani maslahi binafsi ya mchezaji huyo aliyefunga jumla ya mabao 31 katika jumla ya michezo 30 aliyocheza msimu uliopita.

Hawa ni wale waliosajiliwa kiangazi na meneja wa Swansea City Michael Laudrup
    Jonjo Shelvey akitokea Liverpool (£5m)
    Alejandro Pozuelo akitokea Real Betis (undisclosed fee)
    Jose Canas akitokea Real Betis (free)
    Jordi Amat akitokea Espanyol (£2.5m)
    Jonathan de Guzman akitokea Villarreal (season-long loan)
    Gregor Zabret akitokea NK Domzale (undisclosed fee)
    Alex Gogic akitokea Olympiakos (free)
West Ham pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ivory Coast lakini Swansea wakionekana kuwa vinara wa mbio hizo.
 Uwekezaji huo katika kikosi umeonekana kuchagizwa zaidi na meneja Michael Laudrup, ambaye amesema Liberty Stadium itabidi kuimarika katika msimu wa 2013-14 katika muendelezo wa mafanikio ya msimu uliopita.
Swansea ilishinda kikombe cha Capital One kwa kuzifunga Liverpool na Chelsea katika safari ya kuelekea kutwaa taji hilo ambapo wameingia katika michuano ya Europa League huku wakimaliza katika nafasi ya risa katika ligi kuu ya England Premier League.

Eric Abidal ajiunga na Monaco baada ya kuachwa na Barcelona
 Mlinzi wa zamani wa Barcelona Eric Abidal amejiunga tena na klabu yake ya zamani ya Monaco kwa mkataba wa miaka mitatu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 33 alirejea uwanjani mwezi April baada ya kupona maradhi ya Ini yaliyoa anza kumsumbua mwaka 2012.
Hata hivyo baada ya kurejea klabu yake ya Barcelona ilimuacha huru mwishini mwa msimu baada ya kuitumikia kwa miaka sita Nou Camp.
Abidal, ambaye wakati mwingine hucheza nafasi ya ulinzi wa kati na ulinzi wa kushoto aliaanzia kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Monaco na baadaye kujiunga na Lille kisha ya nyumbani kwao ya Lyon.
Alishinda taji la ligi kuu ya Ufaransa akiwa na Lyon msimu wa 2007 kabla ya kujiunga na Barcelona kwa ada ya pauni milioni £10.
Abidal aligundulika kuwa na tatizo la ini na kuelekea kufanyiwa upasuaji mwezi March mwaka 2011, lakini alirejea baada ya iezi iwili baadaye ambaye alishinda taji la Champions League baada ya Barca kuinyoa Manchester United katika mchezo wa fainali katika dimba la Wembley.
Mwezi April mwaka 2012 aliwekewa ini kutoka kwa ndugu yake.
Monaco inayojengwa tena tayari imeshawasajili nyota wa kimataifa wa Ufaransa Jeremy Toulalan, mlinzi wa Real Madrid Ricardo Carvalho, nyota pacha wa Porto Joao Moutinho na James Rodriguez, mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao kutoka katika klabu ya Atletico Madrid.

Arouna Kone asajiliwa na Everton akitokea Wigan Athletic
Everton imemsajili mshambuliaji wa Wigan Arouna Kone kwa mpango wa makataba wa miaka mitatu baada ya kuafiki kiasi cha pauni milioni £6 kilichotajwa na klabu yake.
Newcastle na Everton wote walifikia kiwango kwa ajili ya mshambulaiji huyo mwenye umri wa miaka 29 lakini mwenyewe Kone amechagua kuelekea Merseyside
Sasa atakutana na meneja Roberto Martinez, ambaye aliihama Wigan baada ya kumalizika kwa msimu uliopita.
Kone alifunga jumla ya mabao 11 ndani ya msimu uliopita katika ligi kuu ya England na michuano ya FA kabla ya kuteremka daraja na kuelekea Championship.
Bosi wa Wigan Owen Coyle alikaririwa wiki iliyopita akisema anatarajia Kone kuihama klabu hiyo na klabu anayokwenda ni Everton.
Martinez ambaye ameanza katika klabu ya Everton msimu uliopita alijiunga na Kone kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Levante ya Hispania kiangazi.
Kone aliwahi kuvichezea vilabu vya Belgiam Lierse SK, Udach Roda JC na PSV nchini Hispania ni katika klabu ya Sevilla.
Hata hivyo ada ya uhamisho haijawekwa wazi.

Mshambuliaji wa Bayern Munich Mario Gomez kujiunga na Fiorentina
 Mshambuliaji wa Bayern Munich Mario Gomez anatazamiwa kuihama klabu yake ambao ndio mabingwa wa Ulaya na kujiunga na Fiorentina.
Ada ya uhamishom wake haijawekwa wazi kwa ajili ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 lakini taarifa za pembeni zinaeleza kuwa klabu hiyo ya Italia italiapa pauni milioni £17.2.
Mtendaji mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge ameuambia mtandao wa klabu hiyo ya Ujerumani
"Ni Mario Gomez mwenyewe aliyetaka kuihama Bayern Munich na kujiunga na Fiorentina,".
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani alikuwa msaada mkubwa kwa klabu yake katika kushinda taji la Ulaya la vilabu , kushinda ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga pamoja na German Cup ndani ya msimu mmoja.
Bayern Munich ilikataa ofa mbalimbali ikiwemo ofa ya vilabu  kama Chelsea na Liverpool katika dirisha la usajili la mwezi januari mwaka 2011.
But he only started nine Bundesliga games during the campaign, and came on as a last-minute substitute in Bayern's 2-1 win over Borussia Dortmund in the Champions League final at Wembley on 25 May.

No comments:

Post a Comment