Wachezaji wa United wakiondoka Yokohama na kuelekea Osaka.
Moyes akionekana ni mwenye furaha akiwa karibu na msaidizi wake Steve Round.
Ferdinand akipiga picha ya mwisho kwa kutumia simu yake ya mkononi kabla ya kuondoka Yokohama hii leo.
Kocha Phil Neville akipiga picha na shabiki kabla ya kupanda treni ya kasi kulekea Osaka.
Kikosi cha David Moyes kimeondoka Yokohama na kuelekea Osaka kwa treni ya mwendo kasi hii leo.
United imeelekea Kusini-Magharibi ya Japan kabla ya mchezo mwingine Ijumaa dhidi ya Cerezo Osaka ikiwa ni baada ya kupoteza mchezo wa pili katika jumla ya michezo mitatu mpaka sasa dhidi ya Yokohama F Marinos hiyo jana.
Mshabiki walifurika huko Yokohama na
Osaka kuwapa mkono wa kwaheri akina Rio Ferdinand na Ryan
Giggs, wakati ambapo meneja Moyes akionekana kuwa katika hali ya kawaida licha ya kiwango kibovu cha kikosin chake katika pre-season.
Kichapo cha 3-2 kutoka kwa Yokohama jana.
Baada ya mchezo wao wa Ijumaa dhidi ya Osaka United wataelekea Hong Kong kucheza na Kitchee kabla ya kukabiliana na AIK mjini Stockholm na baadaye Sevilla katika dimba la Old Trafford.
Ferdinand na Ashley Young wakiwasili Osaka
Giggs.
No comments:
Post a Comment