Kiungo wa AC Milan Kevin Constant akishikwa kwa nyuma na nahodha wake Daniele Bonera kabla ya kuondoka uwanjani katika mchezo wa maandalizi ya kuanza msimu dhidi ya Sassuolo kufuatia kashfa ya kibaguzi dhidi yake.
Kiungo kinda Mario
Piccinocchi wa Milan akichukua nafasi ya Constant, ambaye aliondoka uwanjani baada ya kukumbana na kasfa ya ubaguzi katika mchezo dhidi ya Sassuolo ambao Milan ilichomoza na ushindi wa mabao 2-1.
AC Milan imekumbwa tena na matatizo kwa wachezaji wake kukashifiwa kibaguzi wa rangi na safari hii ikimkumba kiungo Constant raia wa Papua Guinea kutoka kwa mashabiki wa Sassuolo katika mchezo wa kirafiki.
Kama ilivyokuwa kwa Kevin-Prince Boateng kukasirishwa na kutoka uwanjani katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki miezi sita iliyopita , Kiungo mwingine wa Milan Kevin Constant alikumbana na kadhia hiyo ambapo alilazimika kuupiga mpira kwa hasira na kutoka nje katikam mchezo huo wa kirafiki dhidi ya timu mpya katika ligi ya Italia Serie A, Sassuolo.
Tofauti na ilivyokuwa kwa tukio lililo muhusu Boateng ambapo timu nzima ilimfuata nyuma na mchezo kumalizwa, katika tuki oa leo Milan ilifanya mabadiliko ya mchezaji na mchezi huo wa Trofeo TIM kuendelea.
Inadhaniwa kuwa wakati kiungo wa zamani wa Tottenham Boateng alihusihswa na kuwarushia kwa maneno aliyoambaiwa ni tofauti na hii ya leo kwa kiungo huyu mzaliwa wa Ufaransa ambaye ana uraia wa Guinea alionekana kama ametoa maneno ya kuudhi yaani matusi ambayo hata hivyo hayakusikika vizuri na wengine.
Shirikisho la soka la Italia litalazimika kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ambapo makamu wa Rais wa Milan Adriano Galliano amenukuliwa akisema,
'Ubaguzi wa rangi umekithiri na ni kashafa Italia shirikisho linapaswa kupigana nalo na ningependa kukadhia juu ya hilo.
'Lakini sheria inasema inapokuwa limekutokea unatakiwa kumfuata mwamuzi ambaye atamwambia mwamuzi wa akiba ambaye atamripoti mtu aliyehusika kwa polisi ambao ndio wana jukumu la kusimamisha mchezo.
'Tunaungana na kiungo Constant, lakini si sawa kwake kutoka nje ya uwanja, Nilimwambia na kurudia hilo na kuwaandikia kila mmoja, hupaswi kuondoka uwanjani.'
Mchezo huo uliingia katika hatua hiyo kunako dakika ya 34 wakati kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 kuchukua mpira na kuubutua upande wa mashabiki wa timu mwenyeji upande maarufu kama Distinti Nord ambako kulikuwa na mashabiki wa timu hiyo ya Sassuolo katika uwanja wa Mapei wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 20,000 na baadaye kuelekea katika benchi la timu yake na baadaye kuondoka uwanjani.
Huyu ni Kevin-Prince Boateng aliyetoka uwanjani katika mchezo wa kirafiki baina ya AC Milan na Pro Patria mwezi January.
Ujumbe maalum: Boateng akionekana na jezi ya AC Milan iliyokuwa na ujumbe wa kupiga vita ubaguzi katika mchezo wa ligi dhidi ya Siena baada ya tukio la mchezo wa ubaguzi dhidi ya Pro Patria.
No comments:
Post a Comment