Timu saba tayari zimejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu fainali
ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za nyumbani
itakayoandaliwa nchini Afrika Kusini mwaka ujao.
Nigeria imeonekana kujikatia tikiti baada ya kuilaza Ivory Coast 4-1 katika mechi ya awamu ya kwanza.
Ikiwa Nigeria itashinda mechi ya marudiano, basi itakuwa imejihakikishia nafasi katika fainali hizo.
Baada ya kuondolewa katika fainali zilizopita na
Ghana na Niger, Super Eagles ya Nigeria inahitaji ushindi katika mechi
hiyo ili kumaliza ukame wa miaka mitano wa kutoshiriki katika fainali
hizo.
Kocha wa timu hiyo Stephen Keshi amesema
watajiandaa vyema kwa mechi hiyo kwa kuwa itakuwa jambo la kushangaza
ikiwa watapoteza mechi hiyon ya awamu ya pili.
Hata hivyo Ivory coast itakuwa na kibarua kigumu kwa kuwa wachezaji wake watatu walipewa kadi nyekundu.
Ethiopia ni nchi nyingine ambayp inatarajia kujikatia tikiti ya fainlai hizo kwa mara kwanza.
Ethiopia iliilaza Rwanda kwa bao moja kwa bila mjini Adis Ababa.
Baada ya kuilaza Tanzania kwa bao moja kwa bila
Uganda kwa mara nyingine tena huenda ikafuzu kwa fainali hizo ikiwa
itaibuka na ushindi katika mechi ya raundi ya pili.
Lakini Uganda Crane imewahi kupoteza nafasi kama
hiyo wakati wa mechi yao ya mwisho na kocha wa Uganda Milutin Micho
Sredojevic ana wasi wasi sana kuhusiana na wapinzani wao Taifa Stars.
Mali in anafasi nzuri baada ya kuilaza Guinea
3-1 katika mechi ya awamu ya kwaza sawia na Sudan ambayo ilitoka sare
1-1 na Burundi.
Lakini Burkina Faso na mabingwa wa kombe hilo
mwaka wa 2009 Jamuhuri ya Kidewmokrasia ya Congo wanakibarua kigumu
katika mechi zao za mwisho dhidi ya Niger na Congo Brazzaville mtawalia.
No comments:
Post a Comment