Viongozi wa juu wa shirikisho la soka nchini Kenya
FKF, wanachunguzwa na maafisa wa tume ya kupambana na ufisadi kuhusiana
na madai ya kutoweka kwa mamia ya maelfu ya dola pesa za shirikisha
hilo.
Kwa mujibu wa maafisa hao, fedha zilizo zilitolewa na shirikisho la mchezo la soka duniani FIFA na mashirika mengine.
Afisa
mkuu wa uhusiano mwema wa tume hiyo, Yasin Ayila, amesema, tume hiyo
imepokea malalamishi kuwa maafisa hao wametumia vibaya zaidi ya dola
laki nne, mali ya FKF.
''Tumepata habari zote kuhusiana na akaunti na
kila kitu kitachunguzwa, ili ni pamoja na stakabathi zote za benki,
akaunti zote za FKF'' amesema afisa huyo.
Kiongozi wa FKF kutoka mkoa wa Pwani, Hussein
Terry, amewasilisha stakabadhi za benki ambazo aliziwasilisha kwa tume
hiyo, waziri wa michezo Hassan Wario, shirikisha la mchezo wa soka
duniani FIFA na shirikisho la mchezo huo barani Afrika Caf.
Terry aliambatana na afisa mwingine wa FKF kutoka mkoa wa Nyanza Tom Alila, na naibu mwenyekiti wa FKF Sammy Sholei.
Shole pamoja na Alila wamesimamishwa kazi na FKF kwa madai ya kushutumu uongozi wa FKF madai ambayo wameyakanusha.
Watatu hao wanadai kuwa FKF ilipokea dola elfu
mia nne na kumi kupitia akaunti yake na kwa sasa hayajumuishwa kwenye
hesabu rasmi ya shirikisho hilo.
Mwenyekiti wa FKF, Sam Nyamweya amekanusha madai
hayo akisema kuwa stakabadhi hizo ni bandia na kusema kuwa maafisa wa
FKF ambao wanaidhini ya kushughulika na masuala ya fedha ndio
watakaopewa stakabadhi kuhusu fedha zake.
Nyamweya amesema akaunti waliowasilisha kwa tume hiyo sio yao na kuwa tayari wamewasiliana na benki yao kuhusiana na suala hilo.
No comments:
Post a Comment