Timu
ya Taifa ya Uganda (The Cranes) imewasili Dar es Salaam leo tayari kwa
mechi ya kwanza ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa
Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) kati yake na Tanzania (Taifa Stars)
itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
The
Cranes inayofundishwa na Mserbia Sredojvic Micho imetua Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 5.30 asubuhi kwa ndege ya Air
Uganda, na imefikia hoteli ya Sapphire.
Timu
hiyo leo (Julai 11 mwaka huu) itafanya mazoezi saa 9 alasiri kwenye
Uwanja wa Karume, wakati kesho saa 9 alasiri itafanya mazoezi Uwanja wa
Taifa, kabla ya kuipisha Taifa Stars itakayoanza mazoezi saa 10 kamili
jioni.
Taifa
Stars inayofundishwa na Mdenmark Kim Poulsen, na kudhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager, leo kwa mujibu wa program yake haitakuwa na
mazoezi.
Wachezaji
wanaounda The Cranes ni makipa Ismail Watenga, Kimera Ali na Muwonge
Hamza. Mabeki ni Guma Dennis, Kasaaga Richard, Kawooya Fahad, Kisalita
Ayub, Magombe Hakim, Malinga Richard, Mukisa Yusuf, Savio Kabugo na
Wadada Nicholas.
Viungo
ni Ali Feni, Birungi Michael, Frank Kalanda, Hassan Wasswa, Kyeyune
Said, Majwega Brian, Mpande Joseph, Muganga Ronald, Ntege Ivan, Owen
Kasule, wakati washambuliaji ni Edema Patrick, Herman Wasswa na Tonny
Odur.
No comments:
Post a Comment