KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, August 17, 2013

Boussoufa ajiunga na wengine wakali wa Anzhi kuihama klabu hiyo.

Moubarak Boussoufa amekuwa mchezaji wa kwanza kuihama klabu iliyotumia mapesa mengi kuihama klabu yake ya Anzhi Makhachkala baada ya klabu hiyo kuamua kupunguza matumizi.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Morocco amekubali kimsingi kujiunga na Lokomotiv Moscow.

Anzhi imesema katika taarifa yao fupi kuwa Boussoufa atajiunga na Lokomotiv na imemshukuru mchezaji huyo kwa mchango wake ndani ya klabu katika kipindi chote cha utumishi wake.

Lokomotiv imesema imemsajili nyota huyo kwa mkataba wa miaka mitatu.
Boussoufa alijiunga na Anzhi mwaka 2011 akitokea katika klabu ya Anderlecht ya Ubelgiji.
Mmiliki tajiri wa Anzhi bilionea Suleiman Kerimov mapema mwezi huu aliuushitua ulimwengu wa soka duniani kwa taarifa yake ya kutaka kupunguza matumizi ya klabu hiyo katika bajeti yake.

Matokeo yake ni kwamba wachezaji nyota wote ambao wameifanya klabu hiyo kuwa ni klabu yenye matokeo mazuri uwanjani sasa wako sokoni.

Dinamo Moscow Alhamisi imetangaza kuwa kumsajili nahodha wa Anzhi Igor Denisov, kiungo wa zamani wa Chelsea Yury Zhirkov na mshambuliaji Alexander Kokorin.
Kiungo Oleg Shatov amejiunga na Zenit St Petersburg.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto'o, ambaye alijunga na Anzhi kwa dau kubwa la malipo inavyoonekana ni wazi ataelekea katika klabu ya Napoli ya Italia.

No comments:

Post a Comment