Olivier Giroud akifunga goli pekee la Arsenal.
Meneja Arsene Wenger wa Arsenal ameuanza vibaya msimu wa ligi kuu ya England kwa kichapo tosha kutoka kwa Aston Villa ambapo mshambuliaji Christian Benteke akitumia faida ya zawadi ya penati mbili kuizamisha Arsenal.
Washika mitutu ndio waliokuwa wa kwanza kufuarahia mchezo kwa bao la mapema la Olivier Giroud kunako dakika ya sita ya mchezo lakini Villa wakasawazisha dakika 16 baadaye pale ambapo mwamuzi wa mchezo Anthony Taylor
alipoonyesha ishara ya penati baada ya mlinda mlango Wojciech
Szczesny kumfanyia madhambi Gabriel Agbonlahor lakini wakati ambao pia mshambuliaji wa Villa akiruhusiwa kuondoka.
Penati ya Benteke iliokolewa kwa pigo la kwanza na Szczesny lakini Mbeljian akaurejesha wavuni kwa pigo la mpira wa kurudi yaani rebound.
Keiron Gibbs wa Arsenal alilazimika kuondolewa uwanjani baada ya kuvuja damu nyingi kufuatia kugongana na Andreas Weimann wa Villa kunako dakika ya 27 na Alex
Oxlade-Chamberlain kuingia.
Ilikuwa ni siku mbaya kwa Wenger baada ya Benteke kuandika bao lake la pili kwa penati pia kunako dakika ya 61 baada ya Agbonlahor kufanyiwa madhambi na Koscielny kwa mara ya pili ambaye alitolewa dakika 5 baadaye baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njani.
Antonio Luna alipigilia msumari wa mwisho kwa kuandika bao la 3 kunako dakika ya 85 ya mchezo.
Giroud akishangilia goli lake.
Wojciech Szczesny akiokoa penati ya Benteke kabla ya kufungwa kwa pigo la pili la rebound.
Benteke akifunga kwa rebounnd
Kieran Gibbs wa Arsena akivuja damu nginyi akiwa amelela chini kuzuia damu kuvuja zaidi baada ya kugongana na Andreas Weimann wa Aston Villa.
Gibbs akisindikizwa kutoka nje ya uwanja baada ya kupasuka.
No comments:
Post a Comment