KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, August 17, 2013

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast Sio ajiunga na mabingwa wa Uswiz Basel.

Mshambuliaji wa Ivory Coast Giovanni Sio amejiunga na mabingwa wa Uswiz FC Basel akitokea katika klabu ya VfL Wolfsburg inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Ujerumani 'Bundesliga'.

Mshambiliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye alijiunga na Wolfsburg mwezi Januari 2012, ameichezea ligi kuu ya Ujerumani michezo 10 tu akiwa na klabu yake ya VfL.
Mchezo wa mwisho kuichezea klabu yake ilikuwa ni katika mchezo dhidi ya Hanover 96 ambao walichapwa kwa mabao 2-0 mwishoni mwa juma lililopita.
Katika kipindi cha utumishi wake cha miezi 18 katika klabu hiyo amekuwa akihaha kwa mikopo mara mbili katika vilabu vya Ujerumani na Ufaransa vya Augsburg na Sochaux.
Sio mara tatu amekuwa akitokea benchi katika kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast ukiwemo mchezo wa hivi karibuni ambapo walichapwa na Mexico kwa mabao 4-1 defeat huko New Jersey nchini Marekani Jumatano iliyopita.
Mshambuliaji huyo hata hivyo ana uzoefu wa kutosha na ligi ya Uswiz kwani alishaitumikia klabu ya FC Sion kwa miaka mitatu

No comments:

Post a Comment