KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, August 17, 2013

Liverpool kumliza mshambuliaji wa Anzhi, Willian pauni £110,000 kwa wiki endapo Anzhi itakubali ofa yao.

Willian wa Anzhi.
Liverpool wako tayari kuweka ofa kwa ajili ya Willian kwa malipo ya pauni £110,000 kwa wiki ili akatoe huduma Anfield wakati huu ambapo meneja Brendan Rodgers akikaribia kabisa kumnasa nyota huyo wa Anzhi.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 anawezekana kuondoka katika klabu yake ya Anzhi ya Urusi katika kipindi hiki ambacho klabu yake inajaribu kupunguza matumizi na Liverpool imeanza mazungumzo tangu Alhamisi.
epa03805092 Liverpool Manager Brendan Rodgers during their friendly match against Thailand at Rajamangala National Stadium in Bangkok, Thailand, 28 July 2013. Liverpool FC won 3-0.  EPA/RUNGROJ YONGRIT
Confident: Brendan Rodgers is closing in on signing Willian (Picture: Getty)
Malipo hayo ya wiki yanatajwa kuwa yatakuwa ni zaidi ya yale ya sasa katika klabu yake ambayo ni pauni £90,000 kwa wiki na itaharakisha uhamisho huo endapo ada itakapo kuwa imekubalika.

Anzhi inataka pauni milioni £30 kwa ajili ya kumtoa mshambuliaji huyo na Liverpool imejipanga kwa matumizi makubwa ya wachezaji imeshaanza mazungumzo kwa kutaja kiasi cha pauni milioni £25.
Willian alijiunga na Anzhi mwezi January, baada ya kugomea ofa za Chelsea na Tottenham.

No comments:

Post a Comment