Kocha wa Togo Didier Six kusalia
katika benchi mpaka mchezo dhidi ya DR Congo
Didier Six amekubali
kusalia katika benchi la ufundi la Togo katika mchezo wao wa kusaka nafasi ya
kucheza kombe la dunia dhidi ya DR Congo
mwezi September kabla ya kujiuzulu nafasi yake ya ukocha.
Mfaransa
huyo mwezi wa juni alikaririwa akisema anataka kungatuka katika nafasi yake
kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri shirikisho la soka la nchi ya Togo (TFF)
juu ya gharama na kwamba asingeweza kurejea mjini Lome.
Lakini Six na
TFF hatimaye wamemaliza mzozo baina yao na kufikia katika makubalino kuwa kocha
huyo mwenye umri wa miaka 58 kuendelea katika nafasi yake hiyo mpaka katika
mchezo wa mwisho wa kundi I wa kusaka nafasi ya kucheza kombe la dunia.
Togo wako
katika mkia wa kundi hilo ilhali DR Congo wakishika nafasi ya tatu huku kila
timu ikiwa imeshindwa kufuzu kueleka katika michezo ya mwisho ya mtoano ambayo
itaamua mustakabi wa nani kafuzu na nani kashindwa kufanya hivyo.
Mchezo baina
ya timu zote mbili umekosa msisimko kutokana na msimamo wa kundi kwani timu
hazina nafasi na hivyo utakuwa ni mchezo wa kukamilisha ratiba tu na utakuwa
unakamilisha kipindi cha miaka miwili ya utumishi wa kocha huyo ndani ya TFF.
Msemaji wa TFF
Herve Agbodan amesema
"Kocha Didier
Six amerejea kutoka Ulaya lakini amewasilisha orodha ya wachezaji atakao
watumia dhidi ya DR Congo na amekubali kuwepo katika benchi katika mchezo wa
mwisho.
Togo
inatarajiwa kutangaza kikosi chake rasmi wiki ijayo na taarifa za fununu zinasema
kocha huyo amewaacha wachezaji muhimu kama mshambuliaji Emmanuel Adebayor, mlinda
mlango Agassa Kossi kiungo mchezeshaji Alexis Romao.
Cameroon imemuita mlinda mlango Idriss
Kameni kuelekea katika mchezo dhidi ya Libya.
Kocha wa kikosi
cha timu ya taifa ya Cameroon Volker Finke amemuita tena mlinda mlango Idriss
Carlos Kameni katika kikosi chake cha wachezaji 25 kitakacho kabiliana na Libya
mwezi ujao ambao ni mchezo muhimu wa kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la
dunia.
Cameroon inaongoza
kundi ‘I’ kwa alama moja mbele ya Libya.
Finke ameamua
kumwita tena mlinda mlango mzoefu Kameni, ambaye alishiriki katika michuano
miwili ya kombe la dunia iliyopia na michuano mara tano ya fainali za michuano
ya mataifa ya Afrika.
Mlinda mlango
huyo wa Malaga kwa mara ya mwisho kuitumikia timu ya taifa ilikuwa mwezi Septemba
mwaka 2012 pale Cameroon ilipoichapwa bao 2-0 na Cape Verde katika mchezo wa
mkondo wa kwanza wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika.
Pia kocha
huyo amemrejesha kikosini mshambuliaji Idrissou Mohammadou, ambaye ameifungia
magoli sita katika michezo sita ya klabu yake ya FC Kaiserslautern ya nchini
Ujerumani.
Mchezo wa
mwisho kuichezea Cameroon ni mchezo wa pili wa marudiano dhidi ya Cape Verde uliopigwa
mjini Yaounde ambao licha ya Cameroon kushinda kwa mabao 2-1 lakini bado
waliondolewa katika kinyanganyiro cha fainali za mataifa ya Afrika.
Gaetang Bong
na Jean Armel Kana Biyik wote wamerejeshwa kikosini lakini Fabric Olinga ametupwa
katika orodha ya wachezaji wa pembeni.
Katika safu
ya ushambuliaji , Cameroon itakuwa ikiwategemea Samuel Eto'o na Choupo Moting.
Finke hajamwita
mchezaji hata mmoja kutoka katika ligi ya nyumbani.
Kikosi kamili
Walinda mlango : Idriss Carlos Kameni (Malaga,
Spain), Charles Itandje (Konyaspor, Turkey), Sammy Ndjock (Antalyaspor,
Turkey).
Walinzi : Allan Nyom (Grenada, Spain),
Aurelien Chedjou (Galatasaray, Turkey), Benoit Angbwa (Kryla Sovetov Samara,
Russia), Dany Nounkeu (Galatasaray, Turkey), Nicolas Nkoulou (Marseille,
France), Gaetan Bong (Olympiakos, Greece), Jean-Armel Kana-Biyik (Rennes,
France), Benoit Assou-Ekotto (Tottenham, England).
Viungo : Stephan Mbia (Queens Park Rangers,
England), Eyong Enoh (Ajax Amsterdam, Ireland), Jean II Makoun (Rennes,
France), Joel Matip (Schalke 04, Germany), Raoul Cedric Loe (Osasuna, Spain),
Landry Nguemo (Bordeaux, France).
Washambuliaji : Samuel Eto'o (Anzhi Makhachkala,
Russia), Achille Webo (Fenerbahce, Turkey), Aboubakar Oumarou (Vojvodina Novi
Sad, Serbia), Eric-Maxim Choupo Moting (Mayence, Germany), Jacques Zoua
(Hambourg, Germany), Benjamin Moukandjo (Nancy, France), Jean-Marie Dongou (FC
Barcelone, Spain).
Gareth Bale: Spurs inafikiria ofa pinzani na ile ya Real Madrid huenda ikawa ni Manchester United
Tottenham imepokea
ofa mbili zaidi za rekodi ya usajili ya dunia kutoka katika klabu ya Real
Madrid ya pauni milioni £86 ikimuhusisha Gareth Bale.
Madrid moja
ya klabu kigogo cha nchini Hispania iko katika nafasi ya juu yenye lengo la
kumsajili mshambuliaji huyo wa Wells mwenye umri wa miaka 24, lakini bado klabu
yake ya Spurs inasema hakuna makubaliano yaliyofikiwa na Real.
Ombi linguine
la pili bado halijafahamika lakini Manchester United imekuwa ikihusishwa na ofa
hiyo majira haya ya kiangazi.
Wakati huohuo
Spurs imeiambia klabu ya Chelsea kuwa inataka kumsajili mchezaji kutoka katika
klabu hiyo kwa lengo la kuziba nafasi ya Bale.
Walikuwa karibu
kumsajili winga wa kibrazil Willian kama mbadala wa Bale wiki iliyopita kabla
ya pigo la kunyaka saini yake.
Bale, aliyejiunga
na Spurs kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £10 akitokea katika klabu ya Southampton
2007, alitajwa kuwa mchezaji wa mwaka katika maeneo mawili ya mchezaji bora wa
kulipwa na mchezaji bora chama cha waandishi wa habarimsimu uliopita baada ya
kuwafungia vijana wa White Hart Lane jumla ya mabao 26.
Madrid tayari
imeshatumia jumla ya pauni milioni £50 majira haya ya kiangazi kwa kuwasajili
viungo Asier Illarramendi kutoka katika klabu ya Real Sociedad Isco kutoka Malaga
kwa ada za uhamisho za pauni milioni £34 na £23.
Arsene Wenger nataka mchezaji 'special'.
Meneja wa
Arsenal Arsene Wenger amesisitiza kuwa atamchukua mchezaji muhimu tu kuelekea
katika klabu yake ya Arsenal, ikiwa imesalia wiko moja kabla ya dirisha la
usajili halijafungwa
Arsenal kwasasa
bado inaendelea na mawindo ya wakali watatu , wawili kutoka katika klabu ya Real
Madrid ambao ni Karim Benzema na Angel Di Maria, pamoja na Yahan Cabaye wa Newcastle
United.
Amesema hayo
baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham Jumamosi akisema "They
are special and if I want to add something it has to be special."
Katika miezi
ya hivi karibuni kikosi hicho toka pande za London ya kaskazini kilishindwa
kufanya uhamisho wa kumchukua mshambuliaji Luis Suarez wa Liverpool , pamoja na
kushuhudia ofa yao ya pauni milioni £10 ya kumtaka Cabaye ikitupiliwa mbali
huku pia wakihusishwa na mpango wa kutaka huduma ya mshambuliaji wa Manchester
United Wayne Rooney na Gonzalo Higuain, ambaye
alikwenda kujiunga na Napoli akitokea katika klabu ya Madrid.
Mathieu
Flamini inaaminika yuko katika mazungumzo juu ya kurejea ndani ya klabu hiyo
kwa uhamisho huru na hapo kabla alikuwa akifanya mazoezi na washika mitutu hao
wa London katika kipindi chote cha kiangazi.
Kiungo huyo
aliihama Arsenal na kujiunga na AC Milan ya Italia mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment