Kiongozi mpya wa Chama cha Uendeshaji Baiskeli Ulimwenguni – UCI Brian
Cookson ana kibarua kigumu kuhakikisha kuwa hadhi ya mchezo huo ambayo
imechafuliwa kwa muda mrefu inarekebishwa.
Cookson atataraji kuwa mwendesha basikeli aliyekabiliwa na kashfa kubwa
ya matumizi ya dawa za kulevya Lance Armstrong anaweza kutekeleza jukumu
kubwa katika mchakato wa “ukweli na maridhiano” na kusaidia kuponya
vidonda vya mchezo huo.
Cookson alimpiku kiongozi anayeondoka Pat McQuaid katika wadhifa wa
urais wa UCI baada ya mchakato wa uchaguzi uliokumbwa na hisia kali jana
Ijumaa. Wakati Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 62 akitaraji
ushirikiano kamili kutoka kwa McQuaid kama uchunguzi utaanzishwa
kuhusiana na ufisadi ndani ya chama hicho, Armstrong huenda akawa mmoja
wale ambao Cookson atatangulia kuwatolea mwito.
Kukiri Armstrongkwamba alitumia dawa za kusisimua misuli katika taaluma
yake yote, baada ya kupigwa marufuku ya maisha katika mchezo huo mwaka
mmoja uliopita, kuliharibu hata zaidi hadhi ya uendeshaji baisikeli.
Kampeni ya Cookson ilihusu wito wa kuanzishwa shirika la kupambana na
dawa zilizopigwa marufuku michezoni ambalo litakuwa huru bila uhusiano
na UCI, kwa sehemu, kutokana na madai kwamba McQuaid na rais wa zamani
wa UCI Hein Verbruggen walishirikiana katika siku za nyuma, kuficha
habari kuhusu matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku.
No comments:
Post a Comment